Friday, 10 July 2015

Waturuki watoa futari ya zaidi ya Sh. Milioni 30 kwa wa kazi wa DarWafanyakazi wakishusha maboksi yenye futari kwa ajili ya Waislamu wa Ilala jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa taasisi ya Forum For Balance and Sustainable Development, Imamu Faraji Tamimu akisimamia zoezi hilo.


Mratibu wa dini wa ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania, Muhammed Cicek (wa pili kushoto) wakati ugawaji wa futari kwa wakati za Ilala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanawake wa Kiislamu wa Ilala wakisubiri kukabidhiwa futari zao zilizotolewa na ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa taasisi ya Forum For Balance and Sustainable Development, Imamu Faraji Tamimu (kushoto) akizungumza jambo wakati wa utoaji wa futari hizo.
 
 
 
 
Na Seba Nyanga
WAISLAMU wa Uturuki kupitia ubalozi wao nchini Tanzania wametoa futari yenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 30 katika mkoa wa Dar es Salaam, imeelezwa.

Kwa mujibu wa mratibu wa dini wa ubalozi wa Uturuki nchini, Muhammed Cicek, futari hiyoitawanufaisha waumini wa Kiislamu 1800 wa wilaya za Ilala, Kinondoni na Temeke.

Alisema kila wilaya waumini 600 wamefaidika na zoezi hilo ambalo kwa upande wa Ilala lilifanyika katika msikiti wa Masjid Taqwa, ambapo mwakilishihuyo aligawa maboksi ya futari kwa waumini hao.

Akizungumza kabla ya kugawa futari hiyo mwakilishi huyo aliwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuwa na mshikamano miongoni mwao na kuwasaidia wasiojiweza kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Akigawa chakula hicho kwa niaba ya taasisi ya Hasene ya Uturuki,   Cicek alisema kwamba wametoa msaada huo sio kwa sababu ya uwezo mkubwa wa kifedha waliokuwa nao ama umasikini wa Watanzania, bali kuendeleza mshikamano miongoni mwa waumini wa Kiislamu Tanzania.

Cicek aliwataka waislamu wa Tanzania kuwaombea waislamu wengine wanaopoteza maisha kwenye nchi za Palestina, Syria, Iraq na kwingineko.

Naye Mwenyekiti wa taasisi ya Forum For Balance and Sustainable Development, Imamu Faraji Tamimu alitoa rai kwa waislamu nchini kote kuendelea kuwaombea wenzao wa Uturuki kupitia taasisi yao ya Haseni kwa msaada wa chakula walioutoa wakati huu wa Ramadhani.

Wenzetu wa Uturuki wametupa msaada huu sio kwa sababu ni matajiri ila kwa sababu ya moyo wa upendo kwa Waislamu wenzao, alisema Imamu Tamimu.

No comments:

Post a Comment