Saturday, 11 July 2015

Hatimaye Van Persie aondoka Man United na kwenda FenerbahceLONDON, England
HATIMAYE mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Robin van Persie kwenda Fenerbahce umekamilika, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Uturuki.

Mwenyekiti wa Fenerbahce Aziz Yildirim alisema kuwa makubaliano yalikamilika tangu Ijumaa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, leo Jumapili anatarajia kutua Istambul kwa ndege binafsi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za mwisho za usajili wake.

"Tulifanya kazi kwa nguvu, hadi usiku wa manane. Hatima ye tumefanikiwa kumsajili mcheaji huyo," alisema Yildirim alipokaririwa na gazeti moja.

"Uhamisho wa van Persie umefanyika na nyota mmoja zaidi ametua katika timu ya Fenerbahce.

Van Persie Alhamisi alifanyiwa vipimo vya awali vya afya England na alitarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne wa kuitumikia klabu hiyo ya Uturiki, lakini uhamisho rasmi ulikuwa nado haujathibitishwa.

No comments:

Post a Comment