Saturday, 11 July 2015

Iker Casillas aondoka Real Madrid baada ya kuichezea kwa miaka 25Kipa Iker Casillas.
MADRID, Hispania
KLABU ya Porto imekubali mpango wa kumsajili kipa wa Hispania Iker Casillas kutoka Real Madrid.

Casillas,mwenye umri wa miaka 34, aliyebakisha mwaka mmoja aktika mkataba wake, anaondoka Real baada ya miaka 25, ambapo katika kipindi chake alitwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na matano ya La Liga.

Mchezaji huyo anashikilia rekodi ya Hispania kwa kucheza mechi 162 katika timuyake ya taifa na kushinda taji la Ulaya pamoja na lile la dunia.

Kipa wa Manchester United David De Gea, 24, amekuwa akihusishwa na kuhamia Madrid kumbadili Casillas.

Casillas alijiunga na shule ya soka ya Real mwaka 1990, na kuichezea kwa mara ya kwanza mwaka 1999 na kutumia muda wake eote katika klabu hiyo, na kutwaa mataji 17 makubwa.

Aliondolewa katika kikosi cha kwanza na Jose Mourinho katika msimu wa mwaka 2012-13, huku kocha huyo Mreno akimpa nafasi zaidi Diego Lopez.

Katika msimu wa mwaka 2013-14 kocha Carlo Ancelotti alimchezesha Casillas peke yake katika mechi za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na zile za Kombe la Mfalme wakati Real Madrid ikitwaa taji lake la 10 la Ulaya.

Msimu uliopita alichukuliwa kama kipa namba moja lakini ujio wa De Gea unatarajia kumbadili kama kipa namba moja katika Reak madrid na Hispania.

Mataji ya Casillas

3 x Ligi ya Mabingwa (2000, 2002, 2014)
    
2 x Kombe la Mfalme (2011, 2014)
5 x La Liga (2001, 2003, 2007, 2008, 2012)
1 x Klabu Bingwa ya Dunia (2014)
1 x Kombela Dunia (2010)
2 x Kombe la Ulaya (2008, 2012)

Kwaheri ya kuonana:-

Taarifa kamili ya Real Madrid kuhusu kuondoka kwa Casillas:

"Kwa Real Madrid leo ni sikukubwa kuliko zote, kwa ajili ya kushukuru na kutambua mchango wake. Mmoja kati ya makipa bora katika klabu hii sio tu anaondoka, leo kipa bora zaidi katika historia ya klabu na katika historia ya soka la Hispani anaondoka katika hatua mpya ya historia ya maisha yake ya soka.

"Iker Casillas alifanya mambo mengi pamoja na kuwa nahodha wetu na amekuwa gwiji tangu alipowasili hapa kama mtoto akiwa na umri wa miaka tisa ru.

Klabu yetu ina umri wa miaka 113 na Casillas amekuwa akivalia jezi namba 25 katika miaka hiyo. Wakati wa kipindi hicho amekuwa mmoja wa viongozi wazuri na alipata heshima kubwa na upendo kutoka kwa mashabiki."Iker anaondoka, lakini urithi wake utakuwa hapa milele. Mipango yake na uchezaji wake katika mechi 725 aliyecheza ndani ya jezi yetu inangara kwa wale wote wenye ndoto ya kuwa sehemu ya timu hii.

"Ahsante kwa yote Iker uliyofanya. Ahsante kwa kuwa alama ya ubora katika historia yetu. Unaondoka lakini kwa kweli kamwe hatutakusahau na siku zote utakuwa katika moyo wa Real Madrid."

No comments:

Post a Comment