Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI mpya ya michezo ya kubahatisha ya Spoti Pesa ya Kenya imeipiga
jeki timu ya taifa ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 17,
Serengeti Boys, baada ya kutoa sh. Milioni 50.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Kampuni ya SpotiPesa nchini,
Abbas Tarimba aliahidi kutoa kiasi hicho cha fedha wakati wauzinduzi rasmi wa
kampuni hiyo hapa nchini jijini Dar es Salaam jana.
Alisema kampuni yake imetoa fedha hizo ili kumfuta machozi Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ambaye usiku kucha
juzi alisafiri kutoka Dodoma ili kuwahi uzinduzi huo.
Dk Mwakyembe alikuwa Dodoma, ambako juzi bajeti ya wizara yake ya mwaka
2016-17 ilipitishwa.
Serengeti Boys iko Gabon tayari kwa fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon)
kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 17, ambako itaanza kampeni zake kwa
kucheza na mabuingwa watetezi Mali Mei 15.
Awali, akizungumza katika hafla hiyo Dk Mwakyembe alisema kuwa, Serikali
iko pamoja na kampuni hizo na itatoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha
inafikia malengo yake.
Alisema kuwa tayari Tanzania ina akina Mbwana Samatta 22 waliomo
Serengeti Boys, ambapo aliwaeleza SpotiPesa kuwa hawatapata shida ya kusaka
vipaji na kuviendeleza kwani tayari wako wengi.
Awali, Tarimba alisema kuwa kampuni hiyo mbayo ilianzishwa nchini Kenya
mwaka 2014 na ina mataiwi jijini Nairobi na Liverpool nchini Uingereza na sasa
jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kampuni hiyo itakuwa miongoni mwa kampuni tano bora
zitakazokuwa zikiingizia Serikali fedha nyingi kupitia kodi itakazolipa.
Baadhi ya wadau wengine wa soka waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, Makamu wa Rais wa Simba, Nyange Kaburu,
mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania, Chaneta, Annie Kibira, Kaimu Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF), Michael Mwita.
No comments:
Post a Comment