Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya mawakala 200 wa huduma ya Tigo Pesa, wamejishindia zawadi za
fedha taslimu zaidi ya sh milioni 160 kwenye promosheni ya mwezi mmoja
inayojulikana kama ‘Wakala Cash In Promotion’.
Promosheni hiyo ya nchi nzima iliyozinduliwa mwezi uliopita, ililenga
kuwahimiza Mawakala wa Tigo Pesa nchini kufanya miamala kwa wingi ili kuweza
kujishindia zawadi za fedha taslimu.
Akiwakabidhi zawadi washindi wa promosheni hiyo, kaimu mkuu wa Kitengo
cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha alisema, kampuni ya Tigo
inathamini juhudi kubwa zinazofanywa na mawakala na kuongeza kuwa promosheni
hiyo ililenga kuwazadia mawakala kutokana na kazi nzuri wanayoifanya.
“Kampeni hii siyo tu inaonyesha dhamira yetu ya kuwekeza kwenye biashara
lakini pia adhma yetu ya kugawana tunachokipata kutokana na biashara
tunayofanya pamoja na wadau wetu. Promosheni hii ni fursa nyingine ya
kuwazawadia mawakala wetu fedha taslimu na bonasi ambazo tunawaamini zitawapa moyo wa kufanya
kazi kwa bidii zaidi ili kuendelea kufikisha huduma jumuifu za kifedha kwa
wananchi wengi zaidi,” alisema.
Kwa mujibu wa Pesha, pamoja na washindi wengine, washindi wawili wakubwa
kutoka kila Kanda walipatikana ambao ni Suleiman Hussein na Vicky Ibrahim kutoka
Kanda ya Pwani, Peter Myovela na Stivin Katoto kutoka Kanda ya Kusini, Anton
Masawe na Athuman Mbwana kutoka Kanda ya Kaskazini pamona na Harry Lwila na
Joseph Kabeba kutoka Kanda ya Ziwa.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Pesa, Angelica Pesha (kulia) akimkaabidhi Wakala wa Tigo Pesa, Vicky Ibrahim mfano wa hundi yenye thamani ya sh milioni 2.5. |
“Pamoja na washindi 2000 ambao wamejinyakulia zawadi mbali mbali za
fedha taslimu kutokana na juhudi zao, tumepata washindi wengine wawili wakubwa
kutoka katika kila kanda ambao kwa jumla wao ni nane, ambao wameweza kujishindia sh milioni 12 zaidi kutokana na jitihada zao.
Tunawapongeza sana Mawakala
wote ambao wamefanya vizuri na kujishindia zawadi na kwa wale ambao wahakuweza
kushinda waongeze bidii ili waweze kuwa washindi katika promosheni zijazo,”
alisema.
Akipokea zawadi ya sh milioni 3.5, Suleiman Hussein ambaye ni
Wakala kutoka Kanda ya Pwani alisema: “Napenda kuishukuru sana kampuni ya Tigo.
Promosheni hii inaonesha ni kwa kiasi gani sisi mawakala ni kiungo muhimu
kwenye huduma nzima ya Tigo Pesa. Kuibuka mshindi kwenye promosheni hii ni
rahisi sana kwa kuwa unahitajika kufanya kazi kwa bidii tu. Nawashauri Mawakala
wenzangu wafanye kazi kwa bidi, kwani Tigo Pesa inalipa,”
Vicky Ibrahim, Wakala aliyejishindia sh milioni 2.5 alisema
amefurahi kuwa mshindi wa zawadi hiyo na kuwataka wanawake kuwa mawakala wa
Tigo Pesa na wale ambao tayari ni mawakala kuwekeza zaidi na kufanya kazi kwa
bidii kwa kuwa Tigo Pesa inalipa.
“Tigo Pesa imetuwezesha sisi wanawake kujiajiri na kuboresha maisha
yetu. Nawashauri wanawake wenzangu kujiajiri au kujiongezea vipato vyao kupitia
Tigo Pesa. Kwa kuwa Mawakala pia wanaweza kujishindia zawadi kupitia promoshei
hii kama ambavyo mimi nilivyojishi,” alisema.
No comments:
Post a Comment