Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inakamilisha Wiki ya Utumishi wa Umma kwa
kufanya maonesho ya kuonesha shughuli mbalimbali za kila siku wanazozifanya.
TAA ilianza wiki
hiyo ya Utumisi wa Umma kwa Makao Makuu kutembelea idara zao mbalimbali ikiwemo
ile ya Utawala, eneo la kuwasili na kuondokea abiria mashuhuri au VIP la
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Idara ya Usalama,
Uhasibu katika eneo hilo.
Pia Kaimu
Mkurugenzi Mkuu alitembelea eneo la Usalama katika JNIA Terminal Two, Idara ya
Manunuzi, Usalama na kwingineko, ambako alizungumza na wafanyakazi wa idara
hizo, ambao walieleza utendaji wao wa kazi na changamoto wanazokumbana nazo
katika majukumu yao ya kila siku.
Siku inayofuata,
uongozi wa TAA ulikutana na wafanyakazi wa idara zote katika ukumbi wa Kiwanja
cha Ndege cha Terminal One, ambako walidajili matatizo mbalimbali
yanayowakabili na uongozi ulitoa suluhisho la matatizo hayo.
Katika kutimiza
agizo la Serikali la taasisi zake kuadhimisha wiki hiyo kwa kutembelea idara na
kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika kutekeleza majukumu yao
ya siku hadi siku.
Katika
kukamilisha wiki hiyo, TAA jana na kesho ina banda lake nje ya Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambako mbali na vipeperushi,
majarida na mabango yanayoelezea shughuli zao katika idara tofauti tofauti, pia
wapo wafanyakazi wanaotoa maelezo kwa abiria na watu wengine wenye matatizo au
kutaka kujua zaidi utendaji wa taasisi hiyo.
Katika banda hilo
kuna picha kubwa zinazoonesha viwanja mbalimbali vilivyoboreshwa , ambavyo
baadhi yao vilikuwa havina rami lakini sasa vimewekewa rami pamoja na mambo
mengine yanayofanywa na TAA.
Wiki ya Utumishi
wa Umma inamalizika rasmi kesho nchini kote, huku TAA chini ya Kaimu Mkurugenzi
Mkuu, Salim Msangi ikijitahidi kuwaelimisha wasafiri na wananchi kwa ujumla juu
ya taasisi hiyo na idara zake na jinsi zinavyofanya kazi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment