Tuesday, 21 August 2018
TFF Yapitisha Waamuzi 82 Kuchezesha Ligi Kuu Bara
SHIRIKISHO la Soka
Tanzania (TFF) limepitisha majina ya waamuzi 82 kuchezesha Ligi Kuu ya Tanzania
Bara msimu wa mwaka 2018/2019.
Katika orodha hiyo
wapo waamuzi wa kati 30,Waamuzi wasaidizi 46 na Waamuzi 6 wa akiba.
Waamuzi hao ndio
watakaokuwa na jukumu la kucheza mechi zote za Ligi Kuu katika msimu husika.
Na uteuzi huo
umefanyika baada ya mtihani wa vipimo kwa waamuzi hao uliofanyika mjini Dar es
Salaam mapema mwezi huu.
Waamuzi
waliopitishwa ni Athuman Selukala (Arusha), Erick Onoka (Arusha), Alex Magayi
(Dar es Salaam), Elly Sasii (Dar es Salaam), Isihaka Mwalile (Dar es Salaam),
Israel Nkongo (Dar es Salaam), Mbaraka Rashid (Dar es Salaam), Nadim Aloyce
Leonard (Dar es Salaam) na Liston Hiyari (Dar es Salaam).
Wengine ni
Florentina Zabron (Dodoma), Ally Simba (Geita), Amada Simba
(Kagera),Jonesia Rukyaa (Kagera),
Hussein Athumani (Katavi), Shomari Lawi (Kigoma), Alfred Vitares (Kilimanjaro),
Jacob Adongo (Mara) na Benedict Magai (Mbeya).
Wengine ni Athumani
Lazi, (Morogoro), Fikiri Yussuf (Morogoro), Martin Saanya (Morogoro), Abubakar
Mturo (Mtwara), Daniel Warioba (Mwanza), Emmanuel Mwandembwa (Mwanza), Ludovick
Charles (Mwanza), Ahmad Seif Mbaraka (Pwani), Nassoro Mwinchui (Pwani), Jimmy
Fanuel (Shinyanga), Meshack Suda (Singida) na Hance Mabena wa Tanga.
Waamuzi wasaidizi
au washika vibendera waliopitishwa ni Agnes Pantaleo (Arusha), Abdallah Uhako
(Arusha), Gasper Keto (Arusha), Frank Komba (Dar es Salaam), Germina Simon (Dar
es Salaam), Hamisi Chang'walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam),
Iddi Mikongoti (Dar es Salaam) na Kassim Mpanga (Dar es Salaam).
Wengine ni Lulu
Mushi (Dar es Salaam), Omary Kambangwa (Dar es Salaam), Shaffi Mohamed (Dar es
Salaam), Soud Lilla
(Dar es Salaam),
Charles Simon (Dodoma), Godfrey Msakila (Geita), Janet Balama (Iringa), Rashid
Zongo (Iringa), Edgar Lyombo (Kagera) na Grace Wamala (Kagera).
Wamo pia Jamada
Ahmada (Kagera), Athumani Rajab (Kigoma), Soud Hussein (Kigoma), Sylvester
Mwanga (Kilimanjaro), Leonard Mkumbo (Manyara), Robert Ruemeja (Mara), John
Kanyenye (Mbeya), Mashaka Mandembwa (Mbeya), Jesse Erasmo (Morogoro), Nickolas
Makaranga (Morogoro), Consolata Lazaro (Mwanza), Frednand Chacha (Mwanza),
Josephat Masija (Mwanza), Michael Mkongwa (Njombe), Abdallah Rashid (Pwani) na
Kassim Safisha (Pwani).
Wengine ni Khalfani
Sika (Pwani), Japhet Kasiliwa (Rukwa), Joseph Pombe (Shinyanga), Julius Kasitu
(Shinyanga), Makame Mdogo (Shinyanga), Arnold Bugardo (Singida), Justina
Charles (Tabora), Martin Mwaliaje (Tabora), Nestory Livangala (Tabora), Haji
Mwarukuta (Tanga) na Mohamed Mkono (Tanga).
Waamuzi wa akiba
waliopitishwa ni Steven Daudi Makuka (Iringa), Ahmadi Benard Augustino (Mara),
Ally Mkonge (Mtwara), Abdallah Kambuzi (Shinyanga), Shaaban Msangi (Singida) na
Omary Mdoe (Tanga).
Monday, 20 August 2018
Bonanza la Michezo Uchukuzi Kufanyika Jumamosi
Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Kwanza la Michezo la Uchukuzi linatarajia
kufanyika Jumamosi Agosti 25 kwenye viwanja vilivyopo katika jengo la Mamlaka
ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Banana Jijini
Dar es Salaam, imeelezwa.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Sports Club (USC), Mbura Tenga
alisema juzi kuwa, kikao cha viongozi wa Uchukuzi, ambacho kilifanyika Agosti
13 mwaka huu, kiliamua tamasha hilo la michezo kwa ajili ya watumishi wa
Uchukuzi, lifanyike siku hiyo.
Kikao hicho kiliamua kwa kauri moja kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dk Leonard Chamuriho
ndiye atakuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la michezo litakaloanza saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 Asubuhi.
Tenga alisema kuwa tamasha hilo la kwanza pia
litatumika kuzindua mazoezi kwa kila taasisi kwenye maeneo ya kazi pamoja na
mazoezi ya kujiandaa na Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara
za Serikali (Shimiwi).
Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ndilo imeteuliwa
kuwa mratibu wa kwanza wa tamasha hilo la kwanza la michezo kwa Sekta ya
Uchukuzi.
Katibu huyo alisema kuwa katika kuongeza hamsha
hamsha katika tamasha hilo, uongozi wa USC umewaalika waandamizi wa Wizara,
Wakurugenzi Wakuu, Wakurugenzi wa Idara zinazojitegemea, Watendaji Wakuu wa
Wakala za Serikali na Watumishi waliopo chini ya sekta ya Uchukuzi.
Alisema ni matumaini yao kuwa ushiriki wa wahusika
wote watashiriki na kuamsha chachu ya mazoezi na hatimaye kuimarisha afya za
watumishi wa Uchukuzi.
RC Pwani Afungua Mafunzo ya Mpira wa Meza leo
Mwandishi Wetu, Kibaha
Mwandishi Wetu, Kibaha
SERIKALI imesema kuwa itajitahidi kuuendeleza mchezo wa mpira wa meza
katika shule zilizopo mkoani Pwani.
Hayo yalisemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Everest Ndikilo wakati
akifungua mafunzo kwa walimu wa mchezo wa mpira wa meza yanayofanyika katika
shule za Filbert Bayi na kuhudhuriwa na washiriki 25 wanaofundishwa na mkufunzi
kutoka Afrika Kusini, Clement Meyer.
![]() |
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi. |
Ndikilo alisema kuwa atawasiliana na baadhi ya wawekezaji waliopo mkoani
mwake ili kusaidia kukuza mchezo huo mkoani mwake, ombi ambalo alisema kuwa
halitakataliwa.
Alisema bila shaka wawekezaji hao hawatashindwa kumpatia meza 100 na
vifaa vingine kwa ajili ya kuuendeleza mchezo huo katika shule mbalimbali za
mkoani Pwani.
![]() |
Mkufunzi wa mafunzo ya ufundishaji wa Mpira wa Meza, Clement Meyer wa Afrika Kusini. |
Alisema kuwa elimu watakayopata
walimu hao kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, itasaidia kuwaandaa wachezaji
watakaoweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Makamu wa Rsis wa TOC, Henry Tandau. |
“Endapo nchi yetu itakuwa na walimu wengi wa mchezo wa Mpira wa Meza, na
wakatawanywa kwenye shule zetu, ambapo ndiyo kwenye vipaji, basi miaka michache
ijayo tunaweza kuwa na uwakilishi mzuri katika Michezo ya Kimataifa,"
alisema Ndikilo.
Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau
aliwataka viongozi wa michezo nchini kuandaa mpango mkakati kabla ya kuomba
fedha kwa wafadhili mbalimbali.
Alisema kuwa TOC imekuwa ikipata shida sana kupata mipango mikakati ya
vyama au mashirikisho ya michezo, licha ya kamati hiyo kuvitaka vyama
kuwasilisha mipango mkakati yao,
Katibu Mkuu wa TOC
alisema mchezo wa Mpira wa Meza pamoja na kuwa mkongwe hapa Tanzania, bado
vyama vya mchezo huo vya Tanzania Bara na Zanzibar, TTTA na ZTTA wana kazi ya
ziada kuueneza katika mikoa mbalimbali nchini, kuliko kuchezwa Dar Es Salaam,
na Zanzibar tu.
Alisema katika akili
ya kawaida chama cha Kitaifa maana yake ni nchi nzima na siyo sehemu ya nchi
kama inaoonekana kwa sasa. Hata hawa wanamichezo wanaotuwakilisha katika
mashindano ya Kitaifa na Kimataifa wametoka Mikoani.

Alisema kuna jinsi
ya kuwapata wanamichezo bora wa mpira wa meza walioko Mikoani kama kuandaa
mashindano ya Mikoa ambayo kwa sasa tangu awe Katibu Mkuu TOC hajawahi kusikia
yakifanyika. Vile vile jitihada za ziada zifanyike kwa mchezo wa mpira wa meza
kuenezwa katika shule zetu, ambapo ndipo penye vipaji.
Thursday, 16 August 2018
Paul Pogba Anataka Kuikimbia Manchester United
MANCHESTER,
England
PAUL
Pogba (pichani) anataka kuondoka Manchester United na kutua Barcelona licha ya kumaliza
tofauti zake na kocha wa klabu hiyo, Jose Mourinho.
Man
United inasisitiza kuwa mchezaji huyo aliyesajiliwa na klabu hiyo kwa ada, ambayo ni rekodi ya kiasi cha pauni milioni 89
kamwe hatapigwa bei kwa bei yoyote, lakini Pogba moyo wake ameuelekeza katika kuichezea
Barcelona ya Hispania.
Mourinho
anajaribu kumshawishi kiungo huyo kuendelea kukipiga katika klabu hiyo kwa
kumpatia unahodha katika mchezo wa kwanza wa United wa msimu dhidi ya Leicester.
Hatahivyo, uhusiano wao uliingia dosari wakati Pogba aliposema baada ya mchezo
huo kuwa hana mpango wa kujadili hali iliyopo sasa bila ya kupigwa faini.
Sportsmail
inaelewa kuwa Pogba ana nia ya kucheza soka Barcelona ikiwa ndio sababu kubwa
ya Pogba kutaka kuondoka, na kutoelewa na Mourinho sasa imekuwa sababu kubwa.
Inaamini
kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, ambaye hajadai ongezeko la malipo,
anapenda kuhamia Hispania tangu alipokuwa akitoka Juventus miaka miwili
iliyopita.
Hatahivyo,
wakala Mino Raiola alishindwa kuvishawishi vigogo vya soka vya Hispania vya Barcelona
au Real Madrid, baadae ikaibuka Man United na kuweka rekodi ya dunia kwa ada na
kumyankua mchezaji huyo.
Pogba,
25, ambaye awali aliikacha Man United ya Sir Alex Ferguson na kutua Juventus
mwaka 2012,alimwambia makamu mwenyekiti mtendaji wa Old Trafford Ed Woodward na
wachezaji wenzake kuwa anataka kuondoka tena.
Raiola
amekubaliana na Barca maslahi binafsi na mchezaji huyo yenye thamani ya pauni
milioni 89.5 katika kipindi cha zaidi ya miaka mitano, lakini United tayari
imegomea ofa hiyo kutoka kwa timu hiyo ya Catalans na wanatarajia kuendelea
kugomea hadi dirisha la usajili la Hispania litakapofungwa mwishoni mwa mwezi
huu.
Naibu Spika Awataka Wanafunzi Shule za Filbert Bayi Kusoma kwa Bidii ili Kufaulu Vizuri Masomo
Na
Mwandishi Wetu, Zanzibar
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson amewataka
wanafunzi kusoma kwa bidii na kupata matokeo mazuri ili kuzintendea haki juhudi
wanazofanya wazazi wao kuwasomesha katika shule nzuri zenye huduma bora.
Tulia
aliyasema hayo jana mjini hapa wakati alipokutana na wanafunzi wa shule za
Filbert Bayi. ambao wamekuja kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo za
michezo na mafunzo.
![]() |
Naibu Spika wa Bunge la Muungano, Tulia Ackson akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi na walimu wa Shule za Filbert Bayi mjini Zanzibar juzi. |
Alisema
wazazi wanaupendo mkubwa kwa watoto wao na kuhakikisha wanapata elimu bora
katika shule nzuri, hivyo wanafunzi hawanabudi kuonesha shukrani kwa kusoma kwa
bidii ili kupata matokeo mazuri, kwani hawana sababu ya kushindwa kufaulu.
“Nawatakia
kila la heri na sitarajii kabisa mwanafunzi apelekwe katika shule nzuri zenye
elimu bora, alafu ashindwe kufanya vizuru, “alisema Tulia huku akiwapongeza
walimiliki wa shule hizo kwa kuhakikisha wanafunzi wanapat mahitaji yote muhimu
pamoja na elimu bora.
Akizungumza
kwa niaba ya shule hizo, Mkurugenzi msaidizi wa shule, Elizabeth Mjema
alimshukuru Naibu Spika kwa kukutana na kuwatia moyo wanafunzi hao na kuahidi
kufikisha salamu hizo kwa wanafunzi wengine waliobaki shuleni pamoja na viongozi
wote wa shule hiyo.
Zaidi ya wanafunzi 198 wa shule za msingi na
sekondari za Filbert Bayi za Kimara na Mkuza Kibaha, wako kisiwani hapa kwa
mwaliko wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar (SMZ).
Baada
ya ziara ya mafunzo kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria, wanafunzi
na walimu wa shule hizo, Jumamosi watashiriki michezo mbalimbali katika Uwanja
wa Amaan mjini hapa.
Kesho
Ijumaa wanafunzi hao wa shule za Filbert Bayi pamoja na walimu wao watatembelea
Baraza la Wawkilishi baada ya leo kutembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria
ikiwemo kisima cha chini kwa chini, pango la watumwa, fukwe ambako watumwa
walikuwa wakipitishiwa na kupandishwa majahazi baada ya kupigwa bei na
kupelekwa Uarabuni, maskani ya Sultani, Stone Town na Forodhani, ambako
walipata fursa ya kula urojo.
![]() |
Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Tulia Ackson (kulia) akiagana na Mkurugenzi Msaidizi wa Shule za Filbert Bayi, Elizabeth Mjema mjini Zanzibar jana. |
![]() |
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Filbert Bayi wakiingia katika kisima cha chini kwa chini kilichopo Mwangapwani kisiwani Zanzibar leo. |
![]() |
Baadhi ya walimu wa Shule za Filbert Bayi wakiwa ufukwe wa Bahari ya Hindi leo mjini Zanzibar. |

Monday, 13 August 2018
Uchukuzi Sports Yakabidhi Vikombe vya Mei Mosi
![]() |
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Grayson Mwaigombe (watano kushoto) baada ya
kupokea vikombe vya ushindi vya Mashindano ya Mei Mosi 2018 kutoka kwa Makamu
Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Uchukuzi (USC), Hassan Hemed (wanne kulia) Jijini Dar es Salaam jana, Watatu
kulia ni Katibu wa klabu hiyo, Mbura Tenga. (Na Mpigapicha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KLABU ya Michezo ya Uchukuzi imekabidhi rasmi vikombe
vya ushindi wa michezo mbalimbali vya mashindano ya Mei Mosi 2018 yaliyofanyika
mwaka huu mkoani Iringa, ambako pia ilitwaa ubingwa wa jumla.
Makamu Mwenyekiti wa Uchukuzi Sports Club (USC),
Hassan Hemed ndiye aliyekabidhi vikombe
hivyo kwa Mkurugenzi na Utawala na Rasilimali Watu, Grayson Mwaigombe
aliyepokea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi,Ujenzi na Mawasiliano
(Sekta ya Uchukuzi), Dk Leonard Chamuriho.
Katika hafla hiyo fupi iliyofanyi katika wizara
hiyo jijini Dar es Salaam, USC ilikabidhi jumla ya vikombe 13 ilivyovitwaa
katika Mashindano hayo ya Mei Mosi 2018, ambapo katika michezo iliyotwaa nafasi ya
kwanza iibeba jumla ya vikombe saba.
Katika nafasi ya pili, USC ilitwaa vikombe viwili vya
michezo ya netiboli na Kamba kwa wanawake, huku vikombe vya nafasi ya tatu
vilikuwa viwili, ambavyo ni vya Karata kwa wanawake na wanaume.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa USC Mbura Tenga, vikombe
ambavyo klabu yao ilipata kwa kutwaa nafasi ya kwanza ni pamoja na Mbio za
baskeli, bao, drafti na kuvuta kamba vyote kwa wanaume wakati kwa wanawake
ushindi wa kwanza ulikwenda katika michezo ya mbio za baiskeli, draft na bao.
Chamuriho aliipongeza klabu hiyo kwa kutwaa ubingwa
huo na kuwapa muda wa kuijenga zaidi klabu yao hiyo ili iweze kufanya vizuri
katika mashindano mengine.
![]() |
Makamu Mwenyekiti wa USC, Hassan Hemed (kulia) akiwa na wajumbe wengine wa klabu hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi. |
Timu ya Uchukuzi mwaka huu imefanya vizuri zaidi
tofauti na miaka ya nyuma na pia ilitunikiwa cheti cha ushiriki cha Mei Mosi
2018 kama mshindi wa jumla, huku Ofisa Habari Bi Bahati Mollel wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) alitunikiwa cheti maalum cha ushiriki kwa
kutambua usambazaji wa taarifa kwa vyombo vya habari.
Kiboko Amuua Mtalii Aliyetaka Kumpiga Picha
NAIROBI, Kenya
MTALII wa Taiwan amekufa baada ya kushambuliwa na
kiboko kifuani wakati akijaribu kumpiga picha mnyama huyo nchini hapa.
Chang Ming Chuang, 66, alikuwa akimtafuta mnyama
huyo katika mbuga ya Ziwa Naivasha, kilometa 90 kaskazini-magharibi ya mji mkuu
wa nchi hii, Nairobi.
Mtalii mwingine wa pili, naye pia kutoka Taiwan,
aliumia. Watu sita wameuawa na kiboko katika eneo hilo mwaka huu.
Maji ya kina kirefu kimeshuhudia vifaru, mnyama hatari
anayenyosha na hatari, ametoka katika eneo walikohifadhiwa kutokana na kusaka
malisho.
Mamlaka ya Wanyama
polisi ya Kenya waliwatambua watalii hao wawili kuwa ni Wachina lakini waziri
wa mambo ya nje wa Taiwani baadae alithibitisha kuwa walikuwa ni wataiwani.
Kenya haina uhusiano wa moja kwa moja na Taiwani na inakubali madai ya China
dhidi ya kisiwa hicho cha Taiwani.
Mashuhuda walisema muwa wawili hao waliuwa karibu
sana na mnyama huyo jirani na hoteli ya Sopa. Mtu huyo aliyejeruhiwa
alikimbizwa hospitalini akitokwa na damu kibao na baadae iliripotiwa kuwa
amekufa.
Mtalii mwingine wa
pili, aliyejulikana kwa jina la Wu Peng Te, alitibiwa majeraha madogo katika Hospitali
ya Wilaya ya Naivasha.
Mwenyekiti wa Wamiliki wa Boti katika Ziwa Naivasha,
David Kilo alisema kuwa kuongezesha kwa kina cha maji kumepunguza malisho ya
viboko, na kuwalazimisha wanyama hao kutafuta malisho katika mashamba na eneo
la hoteli, na kuongeza kukaribiana na watu.

Viboko, wana meno makali na uzito wao unafikia kilo
2,750 (karibu tani tatu), wanakadiriwa kuua watu 500 kila mwaka barani Afrika.
Utalii unaiingizia
Kenya kiasi cha Sh bilioni 1.2bn (sawa na dola za Marekani milioni 950) kwa
mwaka.
Subscribe to:
Comments (Atom)