Monday, 30 March 2015

Real Madrid wataka kumsajili Gareth Bale kwa pauni Mil.75



LONDON, England
KLABU ya Chelsea imeripotiwa inajiandaa kuilipa Real Madrid kiasi cha pauni Milioni 75 ili kumnasa Gareth Bale (pichani) kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo katika kipindi cha majira haya ya joto.

The Blues imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa na Bale katika wiki chache zilizopita, huku ikidaiwa kukiwa na mazungumzo ya kujitoa Madrid.

Na sasa taarifa zinasema kuwa Chelsea wako tayari kulipa pauni Milioni 75 ili kumnasa mchezaji huyo.

Bale bado anangangania kuwa ana furaha Madrid na anatarajia kuendelea kuichezea timu hiyo, lakini Chelsea ilidokeza kutoa ofa ya pauni 300,000 kwa wiki kwa mchezaji huyo.

Huyo atakuwa mchezaji anayelipwa zaidi Chelsea kuwahi kutokea na hilo halitakuwa tatizo kwa klabu hiyo.

Tiger Woods aporomoka kiubora wa viwango



 
NEW YORK, Marekani
TIGER Woods ameporomoka kiviwango na kwa mara ya kwanza amejikuta yuko nje ya wachezaji 100 bora katika historia ya maisha yake.

Mshindi huyo mara 14 wa mashindano makubwa, ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa katika nafasi ya 100 mwaka 1996 na na baadae kutumia wiki 683 kuwemo katika nafasi ya kwanza duniani, ameporomoka hadi katika nafasi ya 104.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 39, hajacheza tangu alipojitoa katika mashindano ya Farmers Insurance Open Februari 6.

Woods alisema "anatumaini" ya kurejea katika shindano kubwa la kwanza la mwaka, the Masters, litakaloanza Aprili 9.

Baada ya kujitoa katika shindano hilo la Februari huko Torrey Pines kutokana na maumivu ya mgongo, Woods alitangaza kupumzika mchezo huo kwa muda usiojulikana, akielezea kiwango chake mwaka huu kama "hakikubaliki katika mchezo huo ".

Sunday, 29 March 2015

Ujamaa Intellectuals Network watoa msaada kwa watoto yatima


Ubosi pembeni!:Mratibu wa taifa wa taasisi ya Ujamaa Intellectuals Network (UIN), Lusekelo Nelson Mwandemange akipeleka kiroba cha unga katika kituo cha watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif Jumapili.

Na Mwandishi Wetu
TAASISI ya Ujamaa Intellectuals Network (UIN) Jumapili ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga kilichopo Hananasif Kinondoni Moscow jijini Dar es Salaam.

Taasisi hiyo kupitia idara yake ya jamii, ilitoa vifaa hivyo vilivyokabidhiwa kwa kiongozi na mmiliki wa kituo hicho Bi.Zainab Bakari Maunga ni pamoja na unga, sabuni, madaftari, chumvi, juice, mafuta ya kula, mafuta ya kupaka na vitu vingine.

Mratibu taifa wa UIN Lusekelo Mwandemange ndiye aiyekuwa wa kwanza kukabidhi baadhi ya vifaa hiyo kwa Bi. Maunga kabla ya wana taasisi wengine nao kukabidhi baadhi ya vifaa hivyo.

Kituo hicho kina jumla ya watoto yatima 49 huku baadhi yao wakiwa ni wanafunzi wa chekechea, shule ya msingi na watatu wako sekondari.

Akizungumza baada ya kupokea msaada huo Bi. Maunga alishukuru sana kwa msaada huo na alitaka wasamaria wema wengine kujitokeza kuwasaidia kama walivyofanya UIN.

 Naye Mwandemange alisema mbali na msaada huo, UIN pia kina mpango wa kuwasaidia wanafunzi hao watatu wanaosoma sekondari.

Pia aliwataka watu na tasisi zingine kujitokeza kwa wingi kusaidia kituo hicho ili kuhakikisha watoto hao yatima nao wanapata elimu kama watoto wengine.
Mkamiti Mgawe akibeba ndoo ya mafuta ya kula katika kituo cha watoto yatima




   
 





 


Waangalizi wa kimataifa waumwagia sifa uchaguzi Nigeria



ABUJA, Nigeria
WAANGALIZI wa Kimataifa wameumwagia sifa Uchaguzi Mkuu wa Nigeria, licha ya matatizo ya kiufundi yalijitokeza, maandamano na taarifa za vurugu baadhi ya maeneo.

Taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki-ilisema kuwa, sehemu kubwa ya uchaguzi huo ulifanyika kwa amani.

Hatahivyo, upigaji kura uliendelea kwa siku ya pili katika baadhi ya maeneo nchini Nigeria baada ya kutokea matatizo katika vifaa vya kusoma vitambulisho vya kupigia kura.

Mchuano mkali unatarajia kuwa kati ya Rais wa sasa Goodluck Jonathan na mpinzani wake mkubwa Muhammadu Buhari.

Maelfu wa wafuasi wa upinzani huko Rivers State waliandamana kupinga dhidi ya mauaji ya wafanya kampeni na matatizo yaliyojitokeza katika upigaji kura.

Tume ya Uchaguzi ya Nigeria ilisema katika taarifa yake kuwa, kuliwashwa moto huku tume ya uchaguzi ilikuwa ikijaribu kuyafanyia jazu malalamiko hayo.
 
Bwana Ban aliipongeza Nigeria kufanya uchaguzi huo kwa amani, licha ya taarifa kuwa uvamizi wa Boko Haram na watu wengine.

Aliwataka wapiga kura kuendeleza hali ya amani wakati wote wa mchakato huo wa uchaguzi.

Maoni yake yaliungwa mkono na John Kufuor, kiongozi wa Ecowas, ambaye alisema mchakato mzima wa uchaguzi "ulienda kwa amani ".

Bwana Jonathan na magavana kama watatu kutoka katika chama tawala ni miongoni mwa watu chombo vya kusoma alama za vidole kushindwa kusoma vitambulisho vyao vya kupigia kura. 
N
Teknolojia hiyo ilikuwa na lengo la kupunguza msongamano wa watu na kufanya zoezi kwenda haraka.

Mapokezi makubwa yaisubiri timu ya nyika ya Tanzania




Na Mwandishi Wetu
TIMU ya taifa ya riadha ya Tanzania iliyoshiriki mashindano ya mbio za nyika ya dunia nchini China wanarejea Jumatatu kishujaa baada ya kushika nafasi ya sita.

Mwanariadha wa Tanzania, Ismail Juma ndiye aliyeitoa kimasomaso Tanzania baada ya kumaliza wa tisa, huku wengine wakimaliza nje ya nafasi 10 bora.

Mkimbiaji huyo ni bado chipukizi lakini alionesha uwezo mkubwa kwa ufanya vizuri katika mbio hizo.

Mwaka 2017 mbio hizo za dunia zitafanyika nchini Uganda na Tanzania imepania kuanza maandalizi mapema ili kuhakikisha inafanya vizuri zaidi.

Tutajitahidi mwaka 2017 tuiandae timu vizuri ili iweze kufanya vizuri zaidi katika mbio hizo nchini uganda, alisema Katibi Mkuu wa Riadha Tanzania Suleiman Nyambui.

Mwanariadha Fabian Nelson yeye atawasili mapema Jumatatu na ndege ya Qatal saa saba mchana wakati wengine watakuja baadae na Emirates wakiwa na kocha wao Francis John.

Mbali na hao wanariadha wengine waliomo katika timu ya Tanzania ni pamoja na Bazil John, Alphonce Felix na Panga.

Alisema kuwa vijana hao wakifanya mazoezi vizuri wanaweza kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki katika mbio za mita 5,000 na 10,000.

Michezo ya Olimpiki 2016 itafanyika Rio de Jeneiro nchini Brazil.

Nyambui alisema anatarajia wadau mbalimbali wa riadha watajitokeza kutoa mapokezi ya aina yake kwa wanariadha hao ambao wamefanya kile ambacho hakijawahi kufanywa kwa muda mrefu na wanariadha wa Tanzania.