Tuesday, 3 February 2015

Murray arejea katika nne bora


Murray arejea katika nne bora





LONDON, England
LICHA ya kushindwa na Novak Djkovic katika mchezo wa wikiendi iliyopita wa fainali ya mashindano ya Australian Open, Andy Murray amerejea katika wachezaji wane bora duniani wa mchezo wa tenisi.
Andy Murray amerejea katika nne bora ya viwango vya ubora vya ATP baada ya kutokuwepo kwa miezi 12, akimaliza wa pili katika mashindano ya Australian Open Jumapili.
Mscotland huyo aliporomoka kutoka katika nne bora mwaka mmoja uliopita, huku mara moja tu akifanikiwa kutinga robo fainali ya Melbourne mwaka 2014, lakini amerejea katika nafasi hiyo baada ya kumchapa bingwa namba moja duniani Novak Djokovic na kumyima taji kubwa la tatu katika historia yake ya mchezo huo.
Murray alichapwa 7-6 (7-5) 6-7 (4-7) 6-3 6-0 lakini alirejea katika kiwango chake na kupanda nafasi mbili na kuwa nyuma ya Djokovic, Roger Federer na Rafael Nadal.
Milos Raonic alikuwa mchezaji mwingine aliyeweza kuboresha kiwango chake cha ubora kwa nafasi mbili zaidi, akipaa hadi nafasi ya sita baada ya kutupwa nje na Djokovic katika robo fainali.
Muaustralia Nick Kyrgios alifaidika na mashindano hayo kuchezewa katika ardhi ya nyumbani kwao baada ya kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 kupanda hadi nafasi ya 18 kati ya nafasi 35 ikiwa ni mara yake ya pili kucheza robo fainali ya mashindano makubwa.
Mwenzake Bernard Tomic naye amepoteza nafasi ya 18 hadi kuwa wa 48 wakati Stan Wawrinka aliporomoka kwa nafasi tano hadi wa tisa baada ya kushindwa na Djokovic katika hatua ya robo fainali na kumzuia kutetea taji lake.
Kwa upande wa wanawake, Ana Ivanovic aliteleza kutoka nafasi ya tano hadi ya sita baada ya kushindwa na mchezaji kutoka Jamhuri ya Czech Lucie Hradecka katika raundi ya kwanza na Caroline Wozniacki aliyepanda nafasi tatu na kuwemo katika tano bora.
Serena Williams, ambaye hilo ni taji lake la sita la Australian Open lilimsaidia kuendelea kushika usukani huku dada yake Venus alipanda kwa nafasi saba hadi ya 11.

Monday, 2 February 2015

Wateja Airtel kuzawadiwa gari kila siku



·Kupitia huduma ya Airtel Yatosha


Watu wakipita mbele ya moja ya magari yatakayotolewa na Airtel Tanzania kwa washindi wa Aiter Yatosha Zaidi.  Add caption

 

Viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam vilivyopambwa wakati wa uzinduzi wa Airtel Yatosha Zaidi leo

Mpanda pikipiki akifanya manjonjo wakati wa uzinduzi wa shindano la Airtel Yatosha Zaidi jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya magari yatakayoshindanishwa kwa wateja wa Airtel watakaoshiriki shindano la Airtel Yatosha Zaidi wakati wa uzinduzi wa shindano hilo leo katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Gari aina ya Toyota IST likionekana kwa nyuma wakati wa uzinduzi wa shindano la Airtel Yatosha Zaidi.
Mpanda baiskeli akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa shindano la Airtel Yatosha Zaidi. Pembeni ni magari aina ya Toyota IST yatakayoshindaniwa na wateja wa wanaotumia mtandao wa Airtel Tanzania. (Picha Zote na Cosmas Mlekani).
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Airtel Tanzania, leo imezindua promosheni  kabambe ijulikanayo kama Airtel Yatosha Zaidi kwa wateja wanaotumia vifurushi vya Airtel Yatosha kuweza kujishindia gari aina ya Toyota IST kila siku.


Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Masoko ya Airtel Bwana Levi Nyakundi alisema promosheni hiyo ni nafasi ya kipekee kwa wateja wanaojiunga na vifurushi vya Airtel yatosha vya siku, wiki na mwezi kupata faida zaidi kutokana pesa wanazozitumia. 

Alisema kuwa wateja hao watapata zawadi nono kibao kila siku ikiwemo gari la aina ya Toyota IST.

Nia yetu  kuhakikisha tunatoa huduma na bidhaa bora kwa kupitia huduma yetu ya Airtel Yatosha, huku tukiwazawadia wateja wetu zawadi nono, alisema na kuongeza:
Tunaamini promosheni hii itawapatia wateja wetu uzoefu tofauti wakati wote wakitumia huduma zetu za Airtel Yatosha. Zaidi ya wateja wetu kijishindia magari promosheni hii ya Airtel Yatosha Zaidi itawapatia wateja wetu vifurushi zaidi,” aliongeza Nyakundi

Akiongea kuhusu namna ya kushiriki Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi. Beatrice Singano Mallya alisema ili kushiriki kwenye promosheni hii wateja wanatakiwa kuendelea kununua vifurushi vyao vya Yatosha vya siku, wiki na mwenzi.

Alisema hakuna gharama ya ziada, kwa kununua vifurushi vya yatosha tayari utakuwa umeunganishwa kwenye droo ya yatosha zaidi na kupata nafasi ya kujishinidia Toyota IST moja kila siku

Hii ni promosheni ya aina yake ambapo wateja wetu wanazawadiwa kutokana na matumizi yao ya kawaida ya vifurushi vya Yatosha.  tunatoa wito kwa wale ambao hawajajiunga na vifurushi vya Airtel yatosha kufanya hivi na kupata nafasi ya kushinda gari moja kila sikualiongeza  Mallya

Kununua vifurushi vya yatosha wateja wanaweza au  kupiga *149*99#, kunua kwa kupitia huduma ya Airtel Money au kwa kununua vocha ya Airtel yatosha inayopatikana katika maduka yetu nchi nzima

Mwaka Jana Airtel ilizindua huduma ya kisasa ya kibunifu na yenye vifurushi vya gharama nafuu sokoni. Kuzinduliwa kwa promosheni hii ya Airtel yatosha Zaidi ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel ya kutoa huduma bora huku ikiwazawadia wateja wake kwa kutumia huduma zake

Mwisho

Sunday, 1 February 2015

Kocha Ivory Coast awamwagia sifa Algeria


MALABA, Equtorial Guinea
KOCHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast Herve Renard amedai kuwa, wapinzani wao Algeria walikuwa wazuri zaidi yao licha ya kuwafunga bao 3-1 katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Renard ambaye aliwahi kuipa Zambia ubingwa wa michuano hiyo alisema kuwa, kikosi chake jana usiku kilikuwa dhaifu licha ya ushindi huo ulioiwezesha kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Washindi wa mchezo huo ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lililowekwa kimiani na mchezaji mpya wa Manchester City Wilfried Bony, ambaye pia ndiye aliyefunga la pili baada ya Mualgeria El Arbi Hillel Soudani kusawazisha.
Gervinho aliihakikishia Ivory Coast ushindi baada ya kufunga bao la tatu katika dakika za majeruhi katika mchezo huo uliofanyika jijini hapa na kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kusonga mbele.
Renard alisema kuwa wapinzani wao hao kutoka Afrika ya Kaskazini walikuwa wazuri, lakini walishindwa kutumia nafasi zao vizuri.
"Kwa upande wa soka, mbinu, Algeria walikuwa bora zaidi yetu, " alisema Renard alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo.
Naye Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Algeria Christian Gourcuff aliunga mkono maneno ya mwenzake, ambapo alisisitiza kuwa timu iliyoshinda haikuwa bora.
"Hii sio timu bora iliyoshinda. Kwa upande wa mchezo, tulicheza vizuri lakini bahati haikuwa yetu, " alibainisha Gourcuff.
"Wachezaji wa Ivory Coast hawakupata nafasi nyingi. Hawakustahili kushinda."
Gourcuff pia alitupia lawama ubora wa kiwanja, na kusema kuwa lilikuwa kosa lao kukubali kufungwa na Ghana baada ya kukubali bao la dakika za mwisho na kumaliza wa pili katika Kundi C kwani wangeshinda wangekuwa wa kwanza na wangeikwepa Ivory Coast katika robo fainali.
"lakini ikiwa tumecheza mechi 10, lakini haujafungwa mara 10, ni wazi sisi ni timu bora…”
Mwisho.

Black Energy kuendelea kudhamini wavu


Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA)  Augustino Agapa akisalimiana na wachezaji wa timu ya Jeshi Stars.

Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya kinywaji cha Black Energy imeahidi kuendelea kudhamini mashindano ya wavu wa ufukweni nchini ili kuuendeleza mchezo huo.
Black Energy ndio iliyodhamini mashindano ya kwanza ya taifa ya wavu wa ufukweni yaliyofanyika kwenye hoteli ya Mbalamwezi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua timu ya taifa  itakayoshiriki mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika.
Mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es Salaam katika hoteli hiyo na mbali na Tanzania nchi zingine zinazotarajia kushiriki ni pamoja na Djibout, Somalia, Ethiopia. Rwanda na Burundi.
Mkurugemzi wa Black Energy nchini Amir Shanghavi alisema kuwa wataendelea kutoa fedha kwa Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (Tava) ili kiendelea kuandaa mashindano ya wavu wa ufukweni kwani unaweza kuifikisha mbali nchini kimataifa.
Mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika yatafanyika Mikocheni jijini Dar es Salaam kuanzia Februari  15 hadi 19 na Tanzania wanatarajia kuwakilishwa na timu nne zenye wachezaji nane.
Kwa mujibu wa Shanghavi, Black Energy pia ndio itadhamini maandalizi ya timu hizo za taifa za Tanzania kwa kuziweka kambini, kuzipatia vifaa na mahitaji mengine wakati wa maandalizi ya mashindano ya Kanda ya Tano.
Aidha, wachezaji wanaounda timu hizo za Tanzania zitakazowakilisha taifa ni pamoja na Zuhura Ally na Lizi John wa Jeshi Stars wanawak wakati Prisons itaundwa na Hellen Richard na Everyline Alberth.
Kwa wanaume Tanzania itawakilishwa na mabingwa wake timu ya Karafuu ya Zanzibar yenye wachezaji wawili Mohamed Ismail na Farahani Aboubakar huku washindi wa pili Jeshi Stars watakuwa na David Everist na Ford Edward.

Zawadi zaongezeka Ngorongoro Marathoni


https://zaratours.files.wordpress.com/2012/04/546761_10150651371547116_545457115_9874508_1106404433_n.jpg
Baadhi ya wanariadha wakichuana katika mbio za Ngorongoro Marathoni mwaka jana.

Na Mwandishi wetu
WAANDAAJI wa mbio za Ngorongoro Marathoni Kampuni ya Zara Charity mwaka huu wameongeza zawadi kwa washindi wa mbio hizo zitakazofanyika Aprili 18, imeelezwa.
Kwa mujibu wa mratibu wa mbio hizo zinazofanyika kila mwaka Meta Petro, washindi wa mwaka huu kwa wanaume na wanawake wote watapata zwadi sawa tofauti na miaka ya nyuma.
Petro alisema kuwa katika mbio za miaka iliyopita, washindi wakiume walikuwa wakipata zawadi zawadi licha ya kukimbia mbio za umbali mmoja kama zile za kilometa 21.
Alisema kuwa lengo la kuongeza zawadi na kuweka viwango sawa ni kuondoa unyanyapaa na kuweka usawa kati ya wakimbiaji wakike na wale wa kiume ambao hukimbia umbali mmoja.
Alitaja zawadi za mwaka huu kwa mshindi wa kwanza kwa wanaume na wanewake ni kiasi cha Sh. Milioni 1.2 kwa watakaokimbia mbio za nusu marathoni, yaani kilometa 21.
Petro alisema kuwa, mwaka jana mshindi wa kwanza kwa wanaume aliondola na kitita cha Sh. Milioni 1 wakati mshindi wa wanawake alipewa kiasi cha sh. 500,000 tu.
Mwaka huu washindi wa pili bila kujali jinsi zao kila mmoja ataondoka na kiasi cha Sh. 600,000 wakati mwaka jana aliondoka na Sh.500,000 kwa wanaume wakati kwa wanawake alipewa Sh. 300,000
Washindi watatu kila mmoja atakabidhiwa kitisha cha Sh. 400,000 huku washindi wa tano hadi wa  10 kila mmoja anatarajiwa kuondoka na kifuta jasho kimono ambacho hakukitaja.