Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama (kushoto), akimkabidhi zawadi
ya ngao, Theobald Benigius wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi katika
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) katika sherehe ya
kuwaaga Wastaafu baada ya kustaafu kwa mujibu wa sheria na taratibu za Utumishi
wa Umma.
Na
Mwandishi Wetu
WAFANYAKAZI
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wametakiwa kuchapa kazi kwa
bidii ili kurudisha hadhi ya taasisi hiyo.
Hayo
yalisemwa jana na Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi Julius Ndyamukama wakati akiwaaga
wastaafu watatu wa mamlaka hiyo.
Hafla
hiyo ilikuwa mahsusi kwa ajili ya kuwaaga wastaafu kutoka Idara ya Uandisi na
Huduma za Ufundi ya Kiwanja cha Kimataifa cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA),
ambao ni Mhandisi Theobald Benigius, Ernest Kivela na Bertha Kipenda, ambao wamestaafu
kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha akimkabidhi mmoja wa wastaafu wa Idara
ya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa JNIA, Mhandisi Bertha Kipenda zawadi ya
vifaa vya mazoezi katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar
es Salaam.
Alisema
kuwa juhudi, maarifa na upendo ndio vigezo vitatu, ambavyo ni chachu ya
kuipandisha na kuirejesha kileleni taasisi hiyo, ambayo ilianza kupoteza hadhi
mbele ya uso wan chi na jamii, tofauti na huko nyuma, ambako ilikuwa ikifanya
vizuri zaidi.
Alisema
kwa sasa hadhi ya taasisi hiyo imeshuka mbele ya uso wa nchi na kusababisha
baadhi ya kazi ilizokuwa ikizifanya zamani, sasa kufanya na taasisi nyingine.
“Nashauri
tupendane na tuchape kazi kwa bidii, kwani sura yetu kama TAA hapo katikati ilidorora
kwani tumepoteza kazi nyingi, hivyo tukitaka kurudisha hadhi yetu kama
itatakiwa kusukumana, tutafanya hivyo kwa lengo hilo, ingawa najua wapo ambao
hawataki hivyo,” alisema.
Hatahivyo,
amewashukuru watumishi wenzake kwa kumpokea vizuri tangu kuteuliwa kwake
kuongoza taasisi hiyo takribani miezi sita iliyopita, ambapo amewataka
kushirikiana zaidi.
 |
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama, akiongea na watumishi walioudhuria
hafla ya kuwaaga watumishi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi wa Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), waliostaafu hivi karibuni
jijini Dar es Salaam. |
Pia
ameweka angalizo kwa Watumishi wote kuwa muda wote atakaokuwepo hapo kama
Mkurugenzi Mkuu, atalazimika kuwasumbua na kuwasukuma, ili sura ya TAA
iliyopotea, kurejea katika hali yake yazamani.
“Tukitaka kurudisha hadhi yetu kama ilivyokuwa
zamani hivyo itahusu tusukumane na kusumbuana kidogo nitaomba mnivumilie,
lakini lengo likiwa ni kutaka kurudisha TAA ya zamani, ingawa najua wapo
wasiotaka,” alisema.
Aliwapongeza
wastaafu hao na kuwataka kendelea kufanya kazi huko waliko ili kuendelea
kuziimarisha afya zao.
Kwa
upande wake
 |
Kaimu Meneja wa Idara ya Uhandisi na Huduma za
Ufundi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi
Diana Munubi (kushoto), akimkabidhi zawadi picha ya ua Ernest Kevela (wa kwanza
kulia) katika hafla ya kuwaaga wastaafu wa Idara hiyo iliyofanyika hivi
karibuni Jijini Dar es Salaam. |
Mkurugenzi wa JNIA, Paul Rwegasha alisema watumishi hao walikuwa na
nidhamu kubwa na kufanya kazi kwa bidii, pasipo kuchoka wala kuwa na malalamiko,
ambapo amewataka wengine waliobaki kuiga mfano huo uliotukuka.
Lakini,
pia amewataka Wastaafu hao kuendelea kufanya mazoezi kwani wamekuwa wakifanya
kazi ngumu wawapo katika kituo chao cha kazi cha JNIA.
Watumishi kutoka Idara na vitengo
mbalimbali vya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiserebuka kwa
kucheza muziki katika hafla ya kuwaaga watumishi wenzao wa Idara ya Uhandisi na
Huduma za Ufundi waliostaafu hivi karibuni.
Naye
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi
Alex Kalumbete amesema wastaafu hao walikuwa na uvumilivu mkubwa katika
utumishi wa umma kutokana na kazi ngumu walizokuwa wakifanya za kiuhandisi.
Kaimu
Meneja Uhandisi na Huduma ya Ufundi JNIA, Diana Munubi amesisitiza upendo
uendelee kuwepo baina ya watumishi kama vile wastaafu hao walivyokuwa wakiuenzi
wakati wa utumishi wao wote wa umma.
Mmoja
wa wastaafu hao, Bw. Theobald Benigius kwa niaba ya wenzake ameishukuru TAA kwa
kuwezesha kufanya kazi vizuri hadi utumishi wao kukoma kwa kustaafu, na
amewaomba watumishi wenzake kuwa wavumilivu na tabia njema kwani wataweza
kustaafu vizuri
.