Sunday 14 February 2016

Van Gaal apokea kichapo England sasa akimbilia Ligi ya Ulaya




LONDON, England
LOUIS van Gaal alikiri kuwa kufuzu kucheza kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya itakuwa “ngumu sana” baada ya jana kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Sunderland iliyopo katika nafasi ya pili kutoka mkiani na kuongeza presha kwa kocha Manchester United.

Bao la kujifunga la dakika za mwisho kutoka kwa kipa David de Gea katika mchezo uliofanytika kwenye Uwanja wa Mwangaza kuliifanya Man United kufungwa kwa mara ya kwanza na Wearside katika kipindi cha miaka 19.

Kipigo hicho kimewaacha mabingwa hao mara 20 wa Ligi Kuu ya England kuwa pointi sita nyuma ya timu zinazoshika nafasi nne za kwanza zikiwa zimebaki mechi 12 kabla ya liugi kumalizika baada ya nahodha Wayne Rooney kuwa  "hayakuwa matokeo mazuri kabisa ".

Bao la 10 katika msimu la Anthony Martial kuliifanya Man United kusawazisha kabla ya mapumziko, likifuta lile la kuongoza la wapinzani wao lililowekwa kimiani na Wahbi Khazri, lakini Sunderland iliibuka na ushindi katika mchezo huo.

Ushindi huo umezidi kumuweka matatani Van Gaal, huku tetesi zikizagaa kuwa kocha wazamani wa Chelsea Chelsea Jose Mourinho anajiandaa kuchukua mikoba ya Mholanzi huyo mwishoni mwa msimu.

Van Gaal alisema kuwa kumaliza nafasi yanne ni “mahitaji madogo” kwao kwa klabu hiyo ya Man United.

"Ikiwa Wayne alisema itakuwa vigumu kwetu kumaliza katika nafasi nne za juu, baadae nakubalina naye. Itakuwa vigumu sana kutokana na nafasi yenyewe. Bado inawezekana lakini ni ngumu kweli.

"Tulitakiwa kushinda mchezo huu. Tunataka kuwa katika nafasi nne za mwanzo na sasa ni vigumu sana kuwa katika nafasi hiyo. Lakini hilo ndilo lengo letu, hiyo ni nafasi ya chini tunayohitaji kwa klabu kama hii. Huwezi kulifumbia macho hilo.”

United inaweza pia kufuzu kwa Ligi Kuu kwa kushinda Ligi ya Ulaya.
Timu hiyo itaifuata timu ya Denmark ya FC Midtjylland katika hatua ya 32 ya mashindano hayo Alhamisi na Van Gaal aliongeza: "Unaweza kusema ndio. Hiyo ni njia nyingine ya kufuzu. Lakini kuna baadhi ya vikosi vizuri sana vimeachwa katika mashindano hayo.”
 
Ronaldo azidi kumbeba Zidane Real Madrid 
 
MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane ameendelea kumsimu mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo baada ya Mredno huyo kufunga mabao mawili wakati kikosi chake kikiibuka na ushndi wa mabao 4-2 katika mchezo wa La Liga dhidi ya Athletic Bilbao.

Mabao hayo mawili ya Ronaldo yamemfanya kufunga bao moja zaidi ya mfungaji anayeongoza katika La Liga Luis Suarez baada ya kufunga mabao 21 katika mechi 32 alizocheza katika mashindano yote msimu huu.

Hatahivyo, mchezaji huy bora mara tatu wa dunia bado amekosolewa kwa kushindwa kuonesha makali yake ya kufunga mabao katika mechi kubwa za Real Madrid ugeni msimu huu.

"Vyombo vya habari viko hapa kwa ajili ya kuangalia kama Ronaldo anacheza vizuri au vibaya, lakini leo ameonesha mchezo mzuri na uwezo wa kufunga, “alisema Zidane.

"Kwangu mimi Cristiano ni mtu muhimu sana katika nafasi ya wingi. Wakati alipobadilisha mchezo hasa anapokuwa akikabiliana na mchezaji mmoja mmoja.

"Nia ni kucheza na Cristiano zaidi katika ushambuliaji wa pembeni…”

Ushindi huo umemfanya Zidane kuwa na mwanzo mzuri kama kocha wa Real Madrid tangu kuchukua nafasi ya Rafael Benitez mwizi uliopita na kutoka sare katika mechi sita za mwanzo.

Hatahivyo, Mfaransa huyo anakabiliwa na mtihani mkubwa hadi sasa wakati Real Madrid itakaporejea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ugenini dhidi ya Roma Jumatano.

Zaza aizamisha Napoli wakati Juventus ikishika usukani  Italia

ROME, Italia

MCHEZAJI tegemeo la Italia kwa michuano ya fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016, Simone Zaza alifunga bao safi katika dakika za mwisho wakati mabingwa Juventus wakiwa pointi moja mbele kileleni mwa Serie A ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Napoli Jumamosi.

Napoli, hicho ni kipigo chake cha tatu katika kampeni zake za kuwani ubingwa, ilisafiri kaskazini kwa ajili ya michezo miwili dhidi ya mabingwa hao kwa mara ya kwanza tangu katika kampeni za mwaka 2009-2010.

Kwa ushindi huo, Juventus sasa inaongoza katika msimamo wa ligi pamoja na Napoli, ambayo ina saka taji la kwanza tangu mwaka 1990 wakati Diego Maradona alipoiwezesha klabu hiyo ya kusini kutwaa taji lake la pili, sasa ni ya pili na inatofauti ya pointi moja.

Kocha Napoli Sarri wote walikiri kuwa safu ya ulinzi ya Juve ndio ilikuwa chanzo cha wao kufungwa: "Tulikuwa na bahati katika mita 20 mwisho.”

"Miezi nane iliyopita walikuwa pointi 24 nyuma yetu, sasa kama tumelingana.”

No comments:

Post a Comment