Sunday, 14 February 2016

Broos ndiye kocha mpya timu ya taifa ya Cameroon


Kocha mpya wa Cameroon, Hugo Broos.

YOUNDE, Cameroon
SHIRIKISHO la Soka la Cameroon (Fecafoot) imemteua mchezaji wazamani wa kimataifa wa Ubelgiji, Hugo Broos, kama kocha mpya wa tembo hao wasiofungika.

Broos, mwenye umri wa 63, amechukua mikoba hiyo kutoka kwa Volker Finke aliyetimuliwa kutoka katika kibarua hicho tangu Oktoba.

Belinga, aliyekuwa kocha wa muda kwa miezi mitatu, atabaki kuwa msaidizi wa Mbelgiji huyo pamoja na mchezaji wazamani wa Ubelgiji, Sven Vandenbroeck.

Broos, ambaye amefundisha karibu nchi kibao za Ulaya, ni chaguo la kushangaza.
Hakuwemo katika orodha ya Fecafoot ya makocha watano, wakiwemo watatu Wafaransa, Mserbia na Mcameroon mmoja.

Broos ana uzoefu mkubwa kama kocha, alishinda ubingwa wa Ublgiji mara mbili akiwa na klabu ya Brugge na baadae akiwa na Anderlecht. Pia alifurahi kucheza katika timu ya Ugiriki, Uturuki katika miaka ya hivi karibuni.

Kibarua chake cha kwanza na timu hiyo ya Cameroon ni kutaka kuiweka timu hiyo kleleni katika mechi za kufuzu za Mataifa ya Afrika 2017 Kundi M, wakati itakapocheza na mchezo wa kufuzu nyumbani na ugenini dhidi ya Afrika Kusini mwezi ujao.

Pia kocha huyo atakuwa kibaruani wakati Simba hao wasiofungika watakapocheza na Ufaransa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki mwezi Mei.

No comments:

Post a Comment