Saturday, 28 January 2017

Patashika robo fainali Mataifa ya afrika kuanza leo jumamosi Burkina Faso anaanza na Tunisia



Mechi za hatua ya Makundi zimemalizika na tayari tumepata timu zinazoendelea mbele kwenye hatua ya Robo  Fainali:

Robo fainali zinaanza leo Januari 28, 2017:

Timu zilizofanikiwa kuendelea mbele kwenye hatua ya Robo fainali ni pamoja na; Burkinafaso, Tunisia, Senagal, 
Cameroon, Misri, DR Congo na Ghana.

Jumamosi hii, 28/01/2017 tutashuhudia Robo Fainali za kwanza kati ya : 

          Burkinafaso dhidi ya Tunisia saa 12 jioni SS Select 2 (DStv 234)

          Senegal dhidi ya Cameroon saa 3.30 Usiku SS Select 2 (DStv 234)

Wakati Robo Fainali za pili zitafanyika Jumapili ya tarehe 29/01/2017 kati ya 

          DR Congo dhidi ya Ghana saa 12 jioni SS Select 2 (DStv 234)
          Misri dhidi ya Morocco saa  3.30 usiku SS Select 2 (DStv 234)


Matokeo ya Kushangaza

Hakuna aliyetarajia kuwa mabingwa watetetezi (Ivory Coast) wangeondolewa haraka kwenye mashindano haya mapema mno pamoja na kuwa na kikosi chenye wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaofanya vizuri katika ligi mbali mbali duniani.
 Sababu kubwa ukiachilia mfumo wa uchezaji ni kukosekana kwa Ari ya Ushindi na ushindani ndani ya timu. Kikosi cha Ivory Coast kilikosa kiongozi uwanjani na pengine ni kutokana na kustaafu kwa wachezaji wao nguli kama ndugu wawili watokao kwenye familia ya Toure; Yaya na Kolo; Hawa walitegemewa kuleta chachu zaidi kwenye timu na kuleta uongozi ndani ya timu. 

Wachezaji kama Eric Bailly, Wilfried Zaha, Serge Aurier, Wilfried Bony, Max Gradel na Salomon Kalou wote hawa walishindwa kuipatia ushindi timu yao na taifa lao kwa ujumla. Ivory coast imeaga mashindano haya bila kushinda mechi hata moja.

 Kutolewa mapema mno kwa Algeria ni matokeo mengine yaliyoshangaza wengi. Riyad Mahrez alishindwa kabisa kusaidia timu yake na hivyo kushindwa kuthibitisha ubora wake kama mchezaji bora wa Africa kwa mwaka huu.

 Wachezaji wenzake kwama Islam Silmani, Nabil Bentaleb na Yacin Brahimi wote walishindwa kuibeba timu yao. Ngome yao ya ulinzi ilionekana kupwaya na kukosa mawasiliano hasa katika idara ya kiungo cha ukabaji. Algeria walionekana wakicheza kibinafsi Zaidi na kutegemea juhudi binafsi kuliko timu.

 Utabiri Wangu wa Robo Fainali

          BurkinaFaso Vs Tunisia
Tunisia ana nafasi kubwa zaidi ya Burkinafaso kwa kuangalia aina ya wachezaji,uchezaji na matokeo ya mechi zilizo tangulia. Mpaka kufikia robo fainali; Tunusia ameshinda mechi 2 na kupoteza 1 wakati Burkinafaso ameshinda 1 na kutoka sare mbili

          Senegal Vs Cameroon
Senegal ni timu iliyoonyesha mpira mzuri sana katika mashindano haya na wanacheza kitimu Zaidi na wanaonyesha mipango ya ushindi kila wanaposhika mpira. Ninawapa nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Cameroon. Mpaka kufikia Robo fainali; Senegal wameshinda mechi 2 na kutoka sare 1 wakati Cameroon wametoka sare 2 na kushinda 1. Hata hivyo hii ni moja kati ya Robo fainali zuri na ngumu sana; chochote kinaweza kutokea

      Misri Vs Morocco
Moja kati ya Robo fainali ngumu sana; majirani wawili kutoka Africa kaskazini wanakutana, waarabu wawili wanaocheza mpira wa kuvutia na wenye kasi na wanaotumia akili sana. Matokeo yoyote yanaweza tokea, ingawa naona ushindi kuamuliwa kwa mikwaju ya penati. Natoa nafasi kubwa kwa Misri; mpaka kufikia hatua hii Misri ameshinda mechi 2 na kutoka Sare 1 wakati Morocco ameshinda mechi 2 na kupoteza 1

          DRC Congo Vs Ghana

Majirani zetu Congo wameonyesha kiwango kizuri sana cha soka huku wakicheza kwa umoja na maelewano makubwa. Uwezo wao wa kumiliki mpira na uwanja hasa kwenye eneo la kati umewafanya  wawe timu bora kabisa.
 
Ghana nao si haba, wameonekana kucheza kwa umoja ingawa bado kuna hali ya utegemezi kwa baadhi ya wachezaji; hata hivyo ni timu nzuri na yenye kuvutia. Nashawishika kusema hii itakuwa Robo fainali bora pengine kuliko nyingine zote ukizingatia viwango vya uchezaji, mbinu, ufundi na ubora ulioonyeshwa na timu zote mbili
Ninawapa nafasi kubwa sana jirani zetu DRC Congo kufanya vizuri kwenye mchezo huu dhidi yay a Ghana. Mpaka kufikia hatua hii, Congo wameshinda mechi 2 na kutoka sare 1 huku Ghana ikishinda mechi 2 na kupoteza 1
Usikose uhondo huu, Ungana nasi (DStv) kupitia chaneli yetu ya Supersport kushuhudia mechi hizi Live bila chenga ndani ya SS6 na SS Selekti kwa vifurushi vyote

Unangoja nini sasa? Uhondo huu unazidi kunogeshwa na Robo fainali, wahi sasa jipatie king’amuzi chako bora kabisa cha DStv na ushuhudie uhondo huu moja kwa moja kutoka Gaboni bila chenga wala mikwaruzo yeyote ile ndani ya DStv HD kwa shilingi 79,000 tu na malipo ya shilingi 19,975 tu kwa mwezi; DStv Bomba.

Friday, 27 January 2017

Ziara ya wajumbe wa kamati ya bunge uwekezaji wa mitaji ya umma walipotembelea JNIA

Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakipata taarifa mbalimbali za ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakiendelea kuchukua maelezo mbalimbali ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi huo, Mhandisi Mohammed Millanga

 (hayupo pichani).

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Sophia Simba (mwenye sketi ndefu), akiwa na wajumbe wenzake wakikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere.

   Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Albert Obama (mwenye shati la maua mbele), akiongoza wajumbe wa kamati hiyo kukagua ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mhe. Joseph Haule ‘Prof. Jay’, (kulia) akiongozana na Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Mhandisi Mohammed Millanga, walipotembelea jengo hilo hivi karibuni.

Mkurugenzi wa mradi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere Mhandisi Mohammed Millanga (aliyenyoosha mkono), akitoa maelezo ya ujenzi kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) walipotembelea hivi karibuni.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Mhe. Albert Obama (kulia) akiwa na wajumbe wa kamati hiyo walipotembelea maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

Mhandisi Mohammed Millanga (aliyenyoosha mkono), akiwaeleza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, ambapo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), wakiondoka katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, baada ya kutembelea maendeleo ya ujenzi huo. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Disemba 2017.


Wednesday, 25 January 2017

JKT QUEENS YAIDHIBU MBURAHATI QUEENS



Na mwandishi wetu

Ligi ya wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliendelea leo  kwa mchezo kati ya JKT Queens na Mburahati Queens zote za Dar es Salaam zilizo kundi A ,ambapo katika mchezo huo JKT Queens iliifunga Mburahati Queens kwa magoli 4-0, uliofanyika kwenye Uwanja wa Karume, Ilala.

Magoli ya JKT Queen yalifungwa na Fatuma Selemani aliyefunga hat trick mnamo dk 54,80 na 81,huku Zena Rashid akifunga dk 67.





Monday, 23 January 2017

Wenger kikaangoni FA yampa hadi alhamisi kujibu mashtaka yanayomkabili


Mwamuzi wa akiba, Anthony Taylor (kushoto) akimtaka kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kutoka baada ya kutolewa uwanjani na mwamuzi Jonathan Moss (hayuko pichani) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Burnley kwenye Uwanja wa Emirates Stadium jijini London mwishoni mwa wiki.
 

LONDON, England
KOCHA Mkuu wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameshtakiwa na Chama cha Soka (FA) kwa madai ya kutoa lugha chafu na kumsukuma mwamuzi wa akiba wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Burnley.

Wenger alimsukuma mwamuzi msaidizi, Anthony Taylor baada ya kutolewa nje katika mchezo huo,a mbao uliofanyika Jumapili na Arsenal kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kocha huyo alijikuta akitolewa nje baada ya kufoka katika dakika ya 93 kufuatia penalti waliyopewa Burnley, ambao walikuwa nyuma kwa bao 1-0.

Katika mchezo huo, Burnley walifikiri kuwa kwa mara ya pili wangeweza kuondoka na pointi moja ugenini msimu huu baada ya Andre Gray kufunga bao la kusawzisha kwa penalti baada ya Francis Coquelin akiadhibiwa kwa kumchezea vibaya Ashley Barnes.

Hatahivyo, the Gunners ndio walikuwa wa kwanza kupata bao baada ya Shkodran Mustafi kufunga bao la kuongoza katika kipindi cha pili akiunganisha wavuni mpira wa kona iliyochongwa na Mesut Ozil akifunga bao lake la kwanza katika soka la Uingereza.

Alexis Sanchez ndiye aliyekuwa mkombozi wa Arsenal katika mchezo huo baada ya kuudokoa mpira katika dakika ya 98 na kumpita Tom Heaton baada ya Ben Mee kupigiwa filimbi kufuatia kumrushia daruga Laurent Koscielny, ambaye alionekana akiwa katika nafasi ya kuotea.

Kwa upande wa Wenger, 67, kocha huyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo aliomba radhi na amepewa hadi Alhamisi awe amejibu tuhuma hizo.

Taarifa ya FA ilisomeka: "Inadaiwa kuwa katika dakika ya 92, Wenger alitumia lugha chafu au za kukera dhidi ya mwamuzi wa akiba.

"Inadaiwa zaidi kuwa kufuatia kutolewa nje kutoka eneo la ufundi, kocha huyo aliendeleza ujeuri katika njie ya kuingilia katika vyumba vya kubadiishia nguo baada ya kumsukuma mwamuzi msaidizi…”

Baada ya kutakiwa na mwamuzi Jon Moss kwenda kukaa jukwaani, Wenger aliondoka kutoka uwanjani lakini alisimama kati njia ya kuingilia na kugoma kutoka akijaribu kuangalia sehemu iliyobaki ya mchezo kutoka hapo, ambapo Taylor alijaribu kumshawishi kuondoka lakini badala yake alimsukuma mwamuzi huyo msaidizi.