![]() |
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Dkt Masatu Chiguma akipimwa joto
la mwili na Afisa Afya, Yusta Malisa wakati bodi hiyo ilipotembelea Jengo la
Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TB3), kwa ziara ya kikazi.
Na Bahati Mollel, TAA
BODI ya Ushauri (MAB) ya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imeridhishwa na ukaguzi wa abiria
wanaotoka nje ya nchi wanaotumia Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege
cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3).
Mwenyekiti wa MAB, Dk Masatu Chiguma amesema leo mara baada ya kumalizika kwa ziara yao ya kwanza ya kikazi
tangu kuteuliwa kwao hivi karibuni ya wametembelea jengo hilo kuwa maafisa afya
waliopo kwenye Jengo hilo wanafanya ukaguzi kulingana na taratibu zilizowekwa,
ili kuzuia maambukizi ya Homa Kali ya mapafu inayoambukizwa na virusi aina ya
Corona, isiingie nchini.
Dkt Chiguma amesema
tahadhari ya kuzuia ugonjwa huo ulioanzia nchini China na kusambaa kwenye nchi
mbalimbali Duniani, imefanyika ipasavyo kwenye Jengo hilo, baada ya
kulitembelea na kuona, vifaa na utendaji wa watumishi hao wa afya.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (wa kwanza kulia),
akiwasilisha taarifa fupi ya Jengo la Tatu la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB3), kwa Bodi ya Ushauri (MAB) ya Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), ilipotembelea jengo hilo leo.
Akizungumzia jengo hilo,
Dkt Chiguma amesema anaipongeza serikali kwa ujenzi wa jengo hili la kisasa
lenye vifaa vya kimataifa, ambapo uendeshaji wake ni wa hali ya juu.
“Tumepita kuanzia mwanzo
wa jengo hadi mwisho wa jengo na tumejionea namna lilivyo bora na zuri, hata
vifaa vyake ni vya kitaalam sana, ukiangalia eneo la mizigo ni mashine tu
zinafanyakazi pamoja na kuwa na Watumishi
wachache lakini kila kitu kinaongozwa na mashine za kisasa,” amesema.
Hatahivyo, amesema Bodi
imebaini bado katika jengo hili kuna upungufu mkubwa wa watumishi, ambapo sasa
waliopo wengi ni wanaofanya kazi kwa mikataba mifupi na wale wanaendelea
kujifunza (Internship), ambapo ni hatari kwa kuwa sio wakutegemewa zaidi
kutokana kuweza kuondoka wakati wowote watakapopata ajira ya kudumu.
Pia ameitaka menejimenti
ya TAA kuhakikisha inaboresha maslahi ya watumishi ili waendelee kulitunza
jengo hilo kwa kufanya kazi kwa bidii.
Halikadhalika amesema
ulinzi na usalama wa abiria na mizigo yao kwenye Jengo hilo ni wa hali ya juu
na uliopangiliwa vyema, kwa kuanzia abiria anapoingia wakati akisafiri hadi
kufika kwenye ndege, hata mizigo inavyokaguliwa kwa kupitia hatua tano napo
panaridhisha.
![]() |
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri (MAB) ya
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakiangalia ramani ya jengo hilo
wakati wakilitembelea katika ziara ya kikazi iliyofanyika leo.
|
Awali akiwasilisha
ripoti ya ujenzi wa jengo hilo, Mkurugenzi wa JNIA, Paul Rwegasha amesema
wanakabiliwa na changamoto ya gharama kubwa za uendeshaji, ambapo jengo zima kwa
asilimia 100 linatumia umeme wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), na
ukikatika hutumika jenereta ambazo zinatumia mafuta mengi.
Pia amesema wanakabiliwa
na upungufu wa watumishi, ambapo wanalazimika kutumia zamu fupifupi na wengine
waliotoka asubuhi kurudi jioni kuongeza nguvu (supporting).
Okay...
ReplyDeleteThis might sound really creepy, maybe even a little "strange"
HOW would you like it if you could just click "PLAY" to listen to a short, "miracle tone"...
And INSTANTLY bring MORE MONEY into your life???
I'm talking about hundreds... even thousands of dollars!!!
Sounds way too EASY??? Think it's IMPOSSIBLE???
Well then, I've got news for you...
Sometimes the greatest miracles in life are the SIMPLEST!!!
In fact, I'm going to PROVE it to you by letting you listen to a REAL "miracle wealth building tone" I've produced...
(And COMPLETELY RISK FREE).
You just push "PLAY" and watch how money starts piling up around you... starting so fast, you will be surprised...
GO here to enjoy the mysterious "Miracle Money-Magnet Sound Frequency" - it's my gift to you!!!