Thursday 7 June 2018

Sam Wa Ukweli Afariki Dunia Akirekodi Wimbo


Na Mwandishi Wetu
MWANAMZIKI aliyetamba na kibao cha Hata Kwetu Wapo, Sam wa Ukweli amefariki dunia alfajiri ya kuamkia leo  katika hospitali ya Palestina iliyopo wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua ghafla ugonjwa wa tumbo.

Kwa mujibu wa mtayarishaji wa muziki Steve Jobiso, aliyekuwa na Sam kabla hajafariki,  alisema Sam alianza kulalamika maumivu ya tumbo.

Anasema hata hivyo walimpeleka chooni baadaye wakamwacha apumzike, lakini ilipofika usiku hali yake ilianza kubadilika  kubadilika na kufanya wawapigie simu mkewe na ndugu zake, ambao wakamjibu watakuja asubuhi.

Anasema lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya na kusema kwamba anashindwa kupumua, hivyo wakampeleka  katika maabara ndogo maeneo ya Mabibo kwaajili ya vipimo, lakini wakaambiwa wampeleke hospitalini.

Jobiso alisema kuwa baada ya kumfikisha katika hospitali ya Palestina, dakika chache wakaitwa na kuambiwa kwamba Sam tayari ameshafariki.

Sam atakumbukwa zaidi kwa muziki wake ambao, miongoni mwa kazi zake zilizofanya vizuri zaidi, ni Loney,Nawaona, Kisiki na wimbo wake mpya ulikuwa Milele ulikuja kufanya vizuri.

No comments:

Post a Comment