Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA watatu wameteuliwa kuwemo katika Kamisheni
mbalimbali za Kamati ya Olimpiki ya Afrika (Anoca),imeelezwa.
Katibu Mkuu TOC, Filbert Bayi |
Kikao hicho cha Kamati ya Utendaji ya Anoca,
kilifanyika hivi karibuni jijini Abuja, Nigeria, ambapo Katibu Mkuu wa Kamati
ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi aliteuliwa kuwa mjumbe wa Kamisheni ya
Olimpiki ya Tokyo 2020.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Bayi jana,
mwenyekiti wa kamisheni hiyo ni Omar Seydina wa Senegal wakati wajumbe mbali na
Bayi wengine ni Paul Tergat (Kenya), Skander Hachica (Tunisia), Habu Gumel
(Nigeria) na Benjamin Boukpeti (Togo).
Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau ameteuliwa kuwa
mjumbe wa kamisheni ya Masoko na Mawasiliano wakati mjumbe wa TOC, Irine
Mwasanga yumo katika kamisheni ya Wanawake na Michezo.
Taarifa hiyo ilisema kuwa majukumu ya kamati hizo
yatatolewa baadae na ofisi ya Katibu Mkuu wa Anoca.
No comments:
Post a Comment