BARCELONA, Hispania
PHILIPPE Coutinho ameanza kuichezea Barcelona wakati
timu hiyo ikiifunga Espanyol na kutinga nusu fainali ya Kombe la Hispania usiku wa kuamkia leo.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa ada ya pauni milioni
142 akitokea Liverpool aliingia akitokea benchi zikiwa zimebaki dakika 22 kabla
ya mchezo haujamalizika wakati tayari Barcawakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Barcelona imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya
mabao 2-1 baada ya mchezo wa kwanza kufungwa 1-0.
Coutinho nusura angesaidia kupatikana kwa bao, lakini
kipa Pau Lopez aliokoa shuti la Luis Suarez, ambaye awali aliifungia Barca bao
la kuongoza dhidi ya wapinzani wao wa jiji.
Lionel Messi alifunga bao safi la pili wakati
akitimiza mabao 4,000 kwenye uwanja huo wa Nou Camp.
Sevilla, Valencia na Leganes – ambayo iliitoa Real
Madrid Jumatano, ni timu zingine zilizopo katika nne bora.
Kabla ya mchezo huo, beki wa Argentina Javier
Mascherano alitoka nje ya uwanja kuaga, baada ya kukamilisha uhamisho wa kwenda
kucheza China katika klabu ya Hebei China Fortune.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 ambaye aliwahi
kuichezea West Ham na Liverpool alitumia miaka nane katika klabu ya Barca,
akishinda mataji 18 yakiwemo manne ya La Liga na mawili ya Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya.
No comments:
Post a Comment