ACCRA, Ghana
HAYAWI hayawi yamekuwa; hatimaye mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed
Salah ametangazwa kuwa mchezaji bora wa Afrika katika tuzo za Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) zilizofanyika mjini hapa usiku wa jana.
Mchezaji amepewa tuzo hiyo kwa mafanikio aliyoyapata mwaka 2017.
Salah amekuwa na mwaka mzuri sana ndani ya 2017
akizisaidia timu yake ya taifa ya Misri kufuzu Kombe la Dunia, huku akiwa wa pili kwa
mabao katika Ligi Kuu ya England (EPL), ambapo mwaka 2017 alifunga jumla ya mabao 39 na kusaidia mara 18.
Timu ya taifa ya Misri ambao ndio mabingwa wa soka
barani Afrika walitangazwa kuwa timu bora Afrika huku tuzo ya mshambuliaji chipukizi
ikienda kwa kinda raia wa Ivory, Coast Patson Daka.
Wakati Misri wakipata tuzo ya timu bora, kocha wao
Hector Cupper alitwaa tuzo ya kocha bora, huku tuzo ya mwanasoka bora Afrika kwa
upande wa wanawake ikienda kwa Mnigeria Asisat Oshoala.
No comments:
Post a Comment