* Wanafunzi
wakereketwa wa Sayansi na Teknolojia
kuoneshana umwamba
Monday, 8 January 2018
Maelfu ya Wanafunzi Kuchuana Tuzo za Kimataifa za DStv Eutelsat Star
Na Mwandishi Wetu
MSIMU wa saba wa
tuzo maarufu barani Afrika kwa wanafunzi wapenzi wa masomo ya Sayansi na
Teknolojia, DStv Eutelsat Star Awards, umezinduliwa rasmi, ambapo Tanzania
ambayo ilishika nafasi ya pili katika tuzo za mwaka jana kupitia mwanafunzi
Davids Bwana, inatarajia kuongeza nguvu na hatimaye kuibuka kidekea.
Kama ilivyokuwa
siku za nyuma, tuzo hizo zinahusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango lenye
ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait. Wanafunzi wa shule za
sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 wanaruhusiwa kushiriki
kinyang’anyiro hicho kitakachoendelea hadi mwishoni mwa mwezi ujao.
Kwa miaka sita
mfululizo, tuzo hizi zimekuwa chachu kubwa kwa vijana wenye ari ya kuwa
wanasayansi huku zikiangazia ni jinsi gani sayansi ya setelait inavyoweza
kubadilisha maendelea, uchumi, na maisha kwa ujumla ya watu wote ulimwenguli.
Kwa mwaka huu,
washindani watatakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu manufaa yaliyoletwa
na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku hapa ulimwenguni na ni
jinsi gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli zote zinazofanyika
kote duniani.
Kama kawaida, tuzo
hizi zina zawadi kabambe, ambapo mshindi wa Insha atapata fursa ya kuzuru kituo
cha Eutelsat nchini Ufaransa na pia kwenda Guiana kushuhudia mubashara
urushwaji wa setelait angani.
Mshindi wa bango
atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini na kutembelea kituo cha anga
cha nchi hiyo na pia Makao Makuu ya MultiChoice Africa akiwa kama mgeni
maalum. Shule zitakazotoa washindi hao
zitapata zawadi ya kufungia huduma ya DStv bure.
Insha pamoja na
mabango hayo hupitiwa na timu ya watahini wenye uzoefu mkubwa katika hatua
mbili. Hatua ya kwanza ni katika kila nchi inayoshiriki, ambapo kila nchi
huwasilisha mshindi wa Insha na mshindi wa Bango. Hawa wawili huingia kwenye kinyang’anyiro
na washindi kutoka mataifa mengine kote barani afrika.
Washiriki wote
wanaweza kupata fomu za ushiriki kutoka ofisi zote za Multichoice au mtandaoni
kupitia www.dstvstarawards.com. Lugha inayotumika
kwa tuzo hizo ni Kiingereza na kazi zote zitakazowasilishwa zitatathminiwa
kulingana na vigezo mbalimbali ikiwemo ubunifu, usahihi wa maelezo na uhalisia.
Pia kuwa mara ya kwanza washiriki wote wanaweza kutoa maoni na kuwasiliana
kupitia ukurasa maalum wa facebook.
Taarifa zote kuhusu vigezo, zawadi na
nyinginezo zinapatikana katika tovuti maalum ya tuzo hizo ambayo ni: http://www.dstvstarawards.com/about.html
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment