MELBOURNE, Australia
CAROLINE Wozniacki amesema kuwa amefurahishwa kwa
kuwa sasa hataulizwa tena kuhusu kutopata mataji ya mashindano makubwa baada ya
juzi kushinda Australian Open.
Mdenish huyo mwenye umri wa miaka 27, alimchakaza
Simona Halep kwa 7-6 (7-2) 3-6 6-4 katika mchezo wa fainali uliofanyika hapa na
hatimaye kupata taji lake kubwa la kwanza katika majaribio 43.
Licha ya kumaliza mwaka akiwa katika nafasi ya kwanza
duniani mwaka 2010 na 2011, mchezaji huyo alikosa mataji manne makubwa.
"Hata ni mambo mazuri sana kwangu, “alisema
Wozniacki.
"Kuanzia sasa kamwe sitaulizwa maswali kama hayo
tena. Nasubiri maswali, ‘Lini utakwenda kushinda tajila pili?'
Leo Jumatatu, Wozniacki atarejea kileleni katika
viwango vya ubora tangu alipokuwa namba moja kwa mara ya mwisho.
"Ni wazi hilo ni jambo maalum,”aliongeza.
"Nafikiri kuwa bingwa mpya wa mashindano makubwa
na bingwa namba moja kwa ubora dunani ni jambo zuri. Nimefurahishwa sana na
hilo. Kwa kweli ndoto imetimia.”
Wozniacki ni Mdenish wa kwanza kushinda taji kubwa la
mchezaji mmoja mmoja, na kuwa nyuma ya Jana Novotna (45), Marion Bartoli (47)
na Flavia Pennetta (49) ambao walishiriki mara nyingi kabla ya kutwaa mataji
makubwa.
Pia kwa ushindi huo ameondoka na kitita cha pauni
milioni 2.3.
Wozniacki alipongezwa katika mitandao ya kijamii na
Serena Williams, ambaye alishindwa kutetea taji lake la Australian Open miezi
minne kabla ya kujifugua mtoto wake wa kwanza.
No comments:
Post a Comment