Friday, 5 January 2018

Waziri Mwakyembe Azindua Tamthilia Mbili Zitakazorushwa DStv na Maisha Magic Bongo

Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice-Tanzania, Maharage Chande (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Habari, Utamadunia, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe kabla ya uzinduzi wa tamthilia mbili jana usiku Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu, Joyce Fisoo.

Na Mwandishi Wetu
WASANII wametakiwa kufaidika na kazi zao za sanaa, ambapo Serikali pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, wako tayari kuwasaidia.

 Waziri aliyasema hayo jana usiku wakati wa uzinduzi wa Sarafu na Kampuni, ambazo zitaoneshwa na kisimbuzi cha DStv.


Tamthilia hizo zitakuwa zikionekana kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo ili kuwapa burudani zaidi wateja wa DStv.

Mwakyembe alisema kuwa amefurahishwa na kiwango cha hali ya juu kilichooneshwa katika tamthilia hizo mpya, ambazo zote zimebuniwa na kutengenezwa hapa nchini na waigizaji wake, wahariri na waongozaji wote ni Watanzania.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harishon Mwakyembe (katikati) akiwa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisoo (wa pili kulia), Mtendaji Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mwuingereza (kulia) Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande (wa pili kushoto) na Mbunge wa Makete Prof. Norman Sigalla King wakifuatilia kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI 
Pia amewaasa wasanii kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili ya jamii wakati wote wanapofanya kazi zao za sanaa, kwani sanaa ni kioo cha jamii na kwamba ikitumika vibaya inaweza kuwa na athari mbaya kwa jamii yetu.

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice-Tanzania, Maharage Chande alisema Kapuni ni tamthilia iliyojaa vituko na misukosuko, ambavyo ni kivutio kwa watazamaji. Alisema Kapuni imeandaliwa na muandaaji maarufu wa filamu nchini, Leah Mwendamseke na vituko na misukosuko ya mahusiano na usaliti wa kimapenzi.

Tamthilia hizo zitaanza kurushwa hewa kuanzia wiki ijayo katika DStv chaneli 160 – Maisha Magic Bongo.

Tamthilia hiyo imechezwa na waigizaji maarufu akiwemo, Jacqueline Wolper, Gabo, Kajala, Masanja, Jenifer Kyaka (Odama),

Mwanamuziki Quick Rocka, DJ maarufu Rommy Jones na mastaa wengine wengi. 

Wasanii mbalimbali wa tasnia ya filamu hapa nchini wakifuatilia kwa makini tamthilia mpya za Kitanzania – SARAFU na KAPUNI zitakazoonekana katika chanel ya Maisha Magic Bongo kuanzia mwezi huu wakati wa uzinduzi wa tamthilia hizo jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Tamthilia hizo zimeigizwa na wasanii maarufu kama Jacquline Wolper, Gabo, Kajala, Mwanamuziki Quick Rocka, Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Irene Uwoya, Idris Sultan na wengineo.
Chande aliongeza kusema kuwa tamthilia ya Sarafu iliyoandaliwa na John Samwel Isike, nayo ni maridadi iliyobeba marafiki wawili ambao wanaingia kwenye chuki na uadui mkubwa mpaka kuingiza familia zao kwenye hatari, kisa ni fedha zinazozaa kiburi, dharau na anasa za kupitiliza.

 Waigizaji maarufu akiwemo Mohammed Funga Funga ( Mzee Jengua), Mzee Chilo, Elizabeth Michael (Lulu), Hemed Suleiman, Irene Uwoya, Idris Sultan, Yusuph Mlela na mastaa wengineo wamo kwenye tamthilia hiyo.

DStv kupitia chaneli yake mahsusi ya maudhiu ya Kitanzania ya Maisha Magic Bongo imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tasnia ya Sanaa inakua na kuifanya iwe moja ya vyanzo muhimu vya mapato kwa wasanii na hatimaye kuchangia katika uchumi wa nchi yetu.

Chanel ya Maisha Magic Bongo ilianzishawa tarehe 1 Octoba 2015, kwa lengo kuu la kuinua na kukuza vipaji na Sanaa hapa Tanzania na pia kuongeza maudhui ya kitanzania kwa wateja wa DStv.

 Kwa kipindi chote hiki Chanel hii imekuwa kwa haraka sana, ambapo kwa sasa ni miongoni mwa Channel zenye watazamaji wengi zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki. Channel hii imekuwa kitovu cha maendeleo ya wasanii hapa nchini, huku mamia ya wasanii wakipata fursa mbalimbali kutokana na kazi zao kurushwa katika channel hii na pia kupata mafuzo na kipato kupitia Sanaa.

Kwa upande wa tasnia ya filamu na uigizaji, Maisha Magic Bongo imeleta mapinduzi makubwa na miongoni mwa filamu zinazotikisa katika soko kwa sasa ni pamoja na Tamthila ya HUBA,ambayo ilipokelewa vizuri sana na Watanzania, pia kuna filamu na vipindi vingine kama MWANTUMU, HARUSI YETU, KITIMTIM ambazo zote zinazidi kuwa maarufu kila uchao.


Kuingizwa kwa tamthilia mpya za Kapuni na Sarafu, nu muendelezo wa mkakati wa Chaneli hii kuongeza maudhui ya kitanzania, na kuwapa watanzania burudani inayoendana na wakati na yenye kuakisi maisha halisi ya kitanzania.

No comments:

Post a Comment