LONDON, England
STOKE City imemteua kocha wazamani wa Aston Villa na
Norwich Paul Lambert kuifundisha timu hiyo, imeelezwa.
Raia huyo wa Scotland mwenye umri wa miaka 48 ametia
saini mkataba wa miaka miwili na nusu wa kuifundisha timu hiyo.
Atachukua mikoba ya Mark Hughes aliyetupiwa virago
mwezi uliopita.
Stoke City katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wako
katika nafasi ya 18, ambapo wanahitaji pointi moja tu ilikuweza kujinasua
kutoka kutoka katika hatari ya ukanda wa kushuka daraja. Waliondolewa katika
Kombe la FA baada ya kuchapwa na Coventry City.
Mechi yake ya kwanza kwenye usukani itakuwa mechi ya
nyumbani dhidi ya Huddersfield Jumamosi.
Lambert amekuwa bila kazi tangu kuondoka katika klabu
ya Wolves mwishoni mwa msimu uliopita.
Amewahi kuwa mkufunzi Colchester, Wycombe Wanderers
na Blackburn.
Alipokuwa mchezaji, alishinda mataji ya Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya akiwa na Borussia Dortmund mwaka 1997 na akashinda mataji manne ya
ligi nchini Scotland akiwa na Celtics.
Aliichezea timu ya taifa ya Scotland mechi 40.
No comments:
Post a Comment