TAIPEI, Taiwan
MAHAKAMA Kuu nchini Taiwan imemuamuru mtu mmoja
kumlipa mama yake karibu kiasi cha dola milioni 1 (sawa na pauni 710,000) kwa
kumlea na kumsomesha udaktari wa meno.
Mama alisaini mkataba na mtoto wake mwaka 1997, wakati
mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 20, ukieleza kuwa atamlipa mama yake asilimi
60 ya kipato chake cha mwezi endapo atafaulu masomo hayo.
Mama alimburuza mwanae mahakamani baada ya kugoma kumlipa
kwa miaka kadhaa kama walivyokubaliana katika mkataba.
Mtoto huyo alikuwa akidai kuwa ni kosa kwa mama yake
kudai kurejeshewa gharama zake za matunzo ya mtoto huyo, lakini mahakama
ilisisitiza kuwa mkataba huo uni halali na mtoto alitakiwa kumlipa mama yake.
Aliamriwa kumlipa mama huyo gharama zote pamoja na riba.
Mama huyo aliyejulikana kwa jina lake la ukoo la Luo, aliwalea
watoto wake wote wawili yeye mwenyewe baada ya kuachana na mumewe miaka mingi
iliyopita.
Bi Luo alisema alitumia maelfu ya dola kwa kuwatunza
watoto wake hao wa kiume kwa kuwasomesha katika shule ya matibabu ya meno,
lakini mama huyo alikuwa na wasiwasi kuwa hawatakuwa tayari kumlea wakati wa
uzee wake.
Mama huyo alisaini mkataba na watoto wake hao wote wawili
wakikubaliana kuwa watamlipa sehemu ya mapato yao kama malipo kwa ada ya shule,
hadi kiasi cha dola za Marekani milioni 1.7.
Mtoto mkubwa alifikia makubaliano na mama yake na kuweka
mkataba kwa kiasi kidogo, vyombo vya habari vya hapa vilieleza.
Hatahivyo, mtoto mdogo, aliyetambulika kwa jina mmoja la
mwisho la Chu, alidai mahakamni hapo kuwa alikuwa mdogo wakati huo akisaini
mkabata huo, na kutaka mkataba huo uchukuliwe kuwa haukuwa halali.
Bwana Chu pia alidai kuwa alifanya kazi kwa miaka kadha
akatika kriniki ya meno ya mama yake baada ya kuhitimu na alimsaidia mama huyo
kutengeneza fedha zaidi kuliko kiasi alichotakiwa kumlipa.
Msemaji wa Mahakama Kuu alisema majaji walikubaliana kuwa
mkataba huo ulikuwa halali kwani uliingiwa wakati mtoto huyo tayari alikuwa mtu
mzima na hakulazimishwa kufanya hivyo.
Chini ya vifungu vya sheria vya Taiwani, watoto wakiwa
watu wazima wanalazimika kuwahudumia wazazi wao wanapozeeka.
No comments:
Post a Comment