Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WACHOVU wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Stand United ya
Shinyanga (pichani) imewazima wababe wa Yanga, Mbao FC baada ya kuwafunga bao 1-0 katika
mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Mbao FC wiki iliyopita ilitoa kipigo kwa mabingwa
watetezi Yanga baada ya kushinda mabao 2-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, lakini
wamejikuta wakishindwa kuibuka na pointi tatu au moja dhidi ya vibonde Stand
United, ambao kabla ya mchezo huo walikuwa wakikalia mkia na pointi zao 10.
Ushindi huo umeibena Stand United hadi kufikia nafasi ya
11 kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo.
Ushindi huo unaifanya Stand United ifikishe pointi 13
baada ya kucheza mechi 14 na kusogea juu hadi nafasi ya 11 kutoka mkiani kwenye
ligi ya timu 16.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Jacob Adongo
aliyesaidiwa na Hellen Mduma na Martin Mwalyaje, Stand United walipata bao lao
dakika ya 40 likifungwa na Vitalis Mayanga kwa penalti baada ya kipa wa Mbao, Ivan
Rugumandiye kumkamata miguu Landry Ndikumana baada ya wote kuanguka wakati
wanawania mpira ndani ya boksi.
Katika mchezo mwingine leo, Mtibwa Sugar imelazimishwa suluhu
na Njombe Mji FC kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
No comments:
Post a Comment