Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Michezo la Wizara na Idara za Serikali
(Shimiwi) linatarajia kuandaa bonanza kubwa la kwanza la michezo mkoani Dodoma
litakalofanyika mwezi ujao.
Katibu Mkuu wa Shimiwi, Moshi Makuka alisema jana
kuwa, bonanza hilo la michezo ni kwa ajili ya kulitambulisha shirikisho hilo mkoani
humo, hasa ukizingatia ndio Makao Makuu ya nchi na wafanyakazi wengi wa
Serikali wako huko sasa.
Makuka alisema kuwa baada ya Dodoma, bonanza hilo
litahamia jijini Dar es Salaam, ambako wafanyakazi wa Serikali watashiriki
katika michezo mbalimbali.
Alisema kuwa kamati yao ya utendaji ilikutana hivi
karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine ilijadili pia utekelezaji wa akizo la
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan la kufanya mazoezi kila wiki ya pili ya
kila mwezi, ili kuweka fiti afya za wafanyakazi.
Pia walijadili jinsi ya kukiendeleza kiwanja chao cha
Bunju B jijini Dar es Salaam, ambapo mbali na kujenga uwanja wa michezo, pia
kutakuwa na hosteli na kumbi kwa ajili ya shughuli mbalimbali, ambazo
zitawaingizia kipato.
Aidha, kikao hicho kiliunda kamati mbalimbali ikiwemo
ya habari na mawasiliano kwa ajili ya kulitangaza shirikisho hilo kwa wadau
mbalimbali.
Alisema waandishi wa habari za michezo wa Kituo cha
Televisheni cha Taifa (TBC), Jane John na Jessey John na
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bahati
Mollel ni miongoni mwa wanaounda kamati hiyo.
Makuka alisema wanataaluma hao wa habari, ambao
pamoja na kuwa ni wachezaji katika timu za wizara zao, wamekuwa pia wakitoa
michango mikubwa katika kutangaza na kuandika habari za Shimiwi.
Wengine waundao kama hiyo ni pamoja na Itika
Mwankenja (Mwenyekiti), Elias Malima (katibu) na wajumbe ni James Katubuka na
David Kitila.
Kamati ya Utendaji inaundwa na Daniel Mwalusamba
(Menyekiti), Ally Katembo (Makamu Mwenyekiti), Makuka (Katibu Mkuu), Alex Temba
(Katibu Msaidizi), William Mkombozi (Mhazini), Frank Kibona (Mhazini Msaidizi).
Wajumbe ni Appolo Kayungi, Damian Manembe, Seleman
Kifyoga, Assumpta Mwilanga na Aloyce Ngonyani, huku wajumbe wa viti maalum ni
Mariam Kihange na Mwajuma Kisengo.
Wanaounda Kamati ya Mipango ni Mwalusamba (Mwenyekiti), Mkombozi (Katibu) na wajumbe ni Makuka, Ngonyani, Kihange na John
Jambele; huku kamati ya Ufundi inaundwa na Kayungi (Mwenyekiti), Manembe
(Katibu) na wajumbe ni Kisengo na Joyce Benjamin; Kamati ya Nidhamu wapo
Katembo (Mwenyekiti), Temba (Katibu) na wajumbe ni Marcel Katemba na Mwilanga.
Kamati ya usajili itaongozwa na Temba (Mwenyekiti),
Kibona (Katibu) na James Emmanuel (Mjumbe); nayo Sekretarieti ya Uendeshaji
inaundwa na Kihange (mwenyekiti), Kifyoga (Katibu), na wajumbe ni Bahati Magambo, Buya Ndalija, Justo
Mwandelile, Ahmed Chitagu, Peter Lihanjala, Gracia Kyelula, Peter Onono,
Modesta Kaunda, Amina Kakozi, Ismail Ismail, Sophia Mkama na James Emmanuel.
Nayo Kamati ya Huduma za tiba itaongozwa na Joakim
Mwaipaja (Mwenyekiti), Magreth Mtaki (Katibu), na Wajumbe ni Richard Yomba,
Haji Masasi, Jafari Chikoko na Gration Kaizirege.
No comments:
Post a Comment