Na Mwandishi Wetu
SIMBA ya Dar es Salaam, jana ilijikita kileleni mwa
msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuifunga Singida United kwa mabao
4-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba ilianza kuandika bao katika dakika ya tatu
tangu kuanza kwa mchezo baada ya Shizza Kichuya kufunga baada ya kutuliza mpira
na kuujaza wavuni kwa juu.
Dakika nne baadae, Nicolas Gyan nusura afunge, lakini
akiwa katika nafasi nzuri,alipiga mpira nje.
Asante Kwasi akiichezea Simba kwa mara ya kwanza
katika mchezo wa Ligi Kuu tangu ajiunge nayo katika dirisha dogo la usajili
akitokea Lipuli ya Iringa, alifunga katika dakika ya 24.
Wachezaji wa Singida walifikiri mfungaji atakuwa
ameotea na kusita kumzuia na kupatikana kwa bao hilo.
Dakika ya 76 Emmanuel Okwi aliyeingia kipindi cha
pili, aliifungia Simba bao la tatu na kuifanya timu hiyo kuzidi kuwa na uhakika
wa kutoka na pointi zote tatu.
Okwi ambaye
alirejea juzi kutoka kwao Uganda, ambako alikaa zaidi ya muda alioruhusiwa,
alifunga bao la nne baada ya kupata pasi kutoka kwa Ndemla baada ya kumkwepa
kipa.
Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha pointi 29
baada ya michezo 13 na kuiacha Azam FC ikisa ya pilina pointi zake 27 huku
Yanga ikibaki katika nafasi ya tano kwa pointi zake 22.
Azam jana ilikalia kwa muda kiti cha uongozi wa ligi
baada ya kutoka sare ya 1-1 na Majimaji ya Songea katika mchezo uliofanyika
kwenye Uwanja wa Majimaji, huku Yanga juzi ikilazimishwa suluhu na Mwadui ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa Taifa.
Kocha moya wa Simba, Mfaransa Pierre Lechantre akifuatilia mpambano wa Ligi Kuu ya Tanzania katika ya Simba na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa. |
Ushindi huo ulishuhudiwa na kocha mpya wa Simba,
Mfaransa Pierre Lechantre aliyekuwa jukwaani wakati timu hiyo ikitoa kipigo
hicho.
Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, klabu hiyo wakati
wowote itaingia mkataba na kocha huyo aliyeipatia Cameroon ubingwa wa Mataifa
ya Afrika (Afcon) mwaka 2000.
Vikosi vilikuwa, Simba: Aishi Manula, Nicholas Gyan,
Asante Kwasi, Juuko Murdhid, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, James Kotei/Mohamed
Ibrahim, Mwinyi Kazimoto, John Bocco, Shiza Kichuya na Mzamiru Yassin/Emmanuel
Okwi.
Singida: Peter Manyika, Micahel Rusheshagonga, Shafik
Batambuzi, Kenned Wilson, Maliki Antiri, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Tafwadza
Kutinyu/Yusuph Kagoma, Lubinda Mundia/Kenny Ally, Kambale Salita na Kiggi
Makasi/Elinywesia Sumbi.
No comments:
Post a Comment