MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wazamani wa Chelsea Diego Costa (pichani) ametambulishwa rasmi katika klabu ya Atletico Madrid na huenda akaanza kuichezea klabu hiyo wiki
hii.
Costa ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Hispania
alikubali kusaini mkataba na klabu hiyo ya La Liga Septemba lakini hakuweza
kucheza kutokana na klabu hiyo kufungiwa kusajili.
"Nilikuwa nikiisubiri kwa muda mrefu siku hii,
nilikuwa nikijaribu kufanya mazoezi na sasa ninahitaji kucheza, “alisema Costa
juzi.
Atletico itacheza dhidi ya Lleida Esportiu kesho katika
mchezo wa Kombe la Mfalme.
Costa juzi alitambulishwa rasmi katika klabu hiyo katika
hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Wanda, pamoja na Mhispania mwenzake Vitolo,
aliyesaini katika timu hiyo akitokea Sevilla Julai.
Baadae alifanya mazoezi ya wazi, ambako vyombo vya habari
vya hapa viliwakilishwa na waandishi 20,000.
"Nimekuwa nikifanya kazi kwa bidii na kujifua kwa
nguvu lakini sikuwa na kitu kingine cha kufanya, “alisema Costa.
"Niko katika kiwango kizuri sana zaidi ya
nilivyowasili hapa, nimejiandaa vizuri na kufanya kazi kwa bidii na kwa sasa
niko tayari kwa kucheza na kuisaidia timu yangu kufunga mabao.”
Atletico Madrid ilikuwa katika kifungo chakusajili kwa
vipindi viwili vya madirisha ya usajili baada ya kuvunja sheria ya usajili
wachezaji wakigeni wenye umri chini ya miaka 18.
Lakini kifungo hicho kimemalizika jana Januari mosi na
hiyo ina maana kuwa Costa anaweza kuanzakuichezea timu hiyo kesho, huku mchezo
wake wa kwanza wa ligi ukiwa Jumamosi nyumbani dhidi ya Getafe.
Costa, ambaye aliondoka Atletico nakujiunga na Chelsea
mwaka 2014, alifunga mabao 59 katika mechi 120 alizoichezea the Blues.
Alirejea Atletico, ambayo iko katika nafasi ya pili ya La
Liga lakini iko pointi tisa nyuma ya vinara Barcelona, ikiwa ni miaka mitatu na
nusu tangu alipoondoka katika klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment