Thursday, 22 September 2016

TAMASHA LA SANAA TANZANIA KUFANYIKA JUMAMOSI SEPTEMBA 24 KIJIJI CHA MAKUMBUSHO DAR ES SALAAM



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMASHA LA SANAA (24 SEPTEMBA 2016)
UTANGULIZI
Siku ya msanii ni mradi uliobuniwa a Baraza la Sanaa la Taifa ukiwa a lengo la KUTAMBUA, KUHAMASISHA na KUTHAMINI kazi na mchango mkubwa unaotolewa na wasanii mbalimbali hapa nchini. Siku hii imeanza kuadhimishwa rasmi hapa nchini kuanzia mwaka 2014 ambapo baadhi ya wasanii waliweza kupewa tuzo na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati huo Mh, Dr. Mohamed Gharib Bilal kutokana na umahiri wao kwenye Sanaa walizozifanya na kuliletea taifa sifa ndani na nje ya Mipaka. Mradi huu umeendelea kukua mwaka hadi mwaka na kuwashirikisha wasanii na wadau wengi Zaidi wa Sanaa hapa nchini kama ambavyo itaendelea kushuhudiwa mwaka huu kwenye maadhimisho ya SIKU YA MSANII 2016.

Msanii wa kizazi kipya Juma Nature anatarajia kufanya mavitu yake kesho Jumamosi katika Siku ya Msanii Makumbusho jijini Dar es Salaam.
 SIKU YA MSANII 2016
Siku ya Msanii mwaka 2016 imejumuisha mtiririko wa matukio ambayo yanakwenda kuakisi kauli mbiu yake ya mwaka huu yaani “NGUVU YA SANAA” Tayari maadhimisho haya yalizinduliwa mnamo tarehe 26 mwezi Mei 2016 kwenye ukumbi wa Alliance Francaise ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Moses Nnauye ambaye aliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel. Uzinduzi huu ulidhihirisha kukua kwa maadhimisho haya kwani yalihusisha mjumuiko wa Sanaa kutoka nchi ya Ufaransa ambapo pia mjumuiko huu utaendelea kwenye matukio mengine yajayo hasa tukio la TAMASHA LA SANAA ambalo linakuja hapo tarehe 24 mwezi Septemba 2016 pale kwenye viwanja vya kijiji cha Makumbusho Kijitonyama Dar es salaam.

Maadhimisho ya mwaka huu kilele chake kitakuwa hapo tarehe 29 Oktoba 2016 ambapo wasanii mbalimbali watapewa tuzo ambapo baadhi ya wasanii watakaokuwa wamepitia mchujo mkali wa kitaaluma na vigezo vilivyowekwa watatunukiwa tuzo mbalimbali kuonyesha mchango wao kwenye sekta ya Sanaa na taifa kwa jumla.
Peter Msechu.
TAMASHA LA SANAA
Kwa mara ya kwanza hapa nchini, SIKU YA MSANII inawakutanisha wasanii wa ainza zote nne za Sanaa kwenye eneo moja yaani Sanaa za muziki, filamu, ufundi na maonyesho ili kuonyesha umahiri wao kwa hadhira. Hili ni tamasha la siku nzima yaani kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 3 usiku ambapo kutakuwa na maonyesho ya kazi mbalimbali za Sanaa kama ufundi na maonyesho na baadae kuhitimishwa na burudani mbalimbali za muziki kutoka kwa wanamuziki wa mitindo mbalimbali ya muziki ikiwa na lengo la kuonyesha Nguvu waliyonayo wasanii pale wanapoungana pamoja.
 
SHUGHULI ZITAKAZOKUWEPO
1.     Tamasha hili litapambwa na shughuli mbalimbali ili kuifanya kuwa siku maalum ya wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake kufika na familia zao na wao pia kujionea umahiri wa wasanii wetu nchini. Shughuli zitakazokuwepo ni pamoja na;
2.     Maonyesho ya kazi za Sanaa za ufundi (uchongaji, ufinyanzi, ushonaji, ufinyanzi na nyingine nyingi) siku hii wale wasusi wote maarufu hapa mjini watahamia kwenye tamasha la Sanaa hili hivyo wale kina mama siku hiyo waje makumbusho kusukwa.

3.     Maonyesho maalum ya filamu za kitanzania ambapo pamoja na kuona wadau wa filamu watapata fursa ya kununua filamu kazi zilizotengenezwa na wasanii wetu maarufu hapa nchini.

4.     Burudani ya muziki wa aina zote utakuwepo huku ukisindikizwa na burudani kutoka kwa ma DJ maarufu wa enzi hizo wakishirikiana na ma DJ wa sasa ili kuhakikisha wadau wanapata burudani isiyochosha kwa siku nzima.

5.     Kutakuwa pia na huduma ya chakula na vinywaji kuanzia asubuhi mpaka jioni ili watu watakaofika kwenye viwanja vya makumbusho waweze kupata huduma zote kusindikizia burudani itakayokuwepo hapo.

Huduma ya utoaji damu itakuwepo.
6.     Kutakuwa na huduma ya uchangiaji damu
7.     Kutakuwa na Jukwaa la Sanaa ambalo litaongozwa na BASATA na Cosota katika kutoa elimu kwa wasanii mbalimbali

8.     Kutakuwa na elimu ya mifuko ya jamii kwa wasanii na jamii ambayo itakuja katika Tamasha

Ifakara Band ni miongoni mwa makundi yatakayotoa burudani ya muziki wa dansi.
BURUDANI
Tamasha hili litashehenezwa na wasanii wa muziki mbalimbali kama ifuatavyo;
Bongo fleva;            Juma Kassim Nature
                                    Peter Msechu
                                    Misoji na wengine wengi ambao watapanda katika jukwaa

Muziki wa Dasi;     CHAMUDATA All Stars (wasanii maarufu wa zamani wataungana na wasanii wa sasa kutoa burudani)
                                    Ifakara Band
                                    John Kitime
Singeli;                      Amsha Group na makundi mbalimbali ya singeli
Ngoma za Asili;      Mandela Group
                                    Safari Group na sarakasi
Taarab;                      Siza Segere
                                    Super Shine

Komedi/Mchekeshaji;     Mluga luga na wachekeshaji mbalimbali
Ma DJ;                       Dj Ibony Moalim
                                    DJ John Pantalikis
                                    Dancer Athuman DigaDiga
Wanamuziki mbalimbali wa nyimbo za injili pia watatoa burudani kuhamasisha Amani ya nchi yetu.

Mtiririko wote huu wa burudani utawahakikishia wadau mbalimbali wa Sanaa watakaofika kuendelea kuwepo mpaka itakapofikia tamati ya tamasha hili kubwa kabisa la Sanaa hapa nchini.

Wanamuziki wa Nyimbo za Injili watakuwepo kuombea taifa amani.
ENI RASMI
Mgeni rasmi kwenye Tamasha hili la Sanaa atakuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Anastazia Wambura (Mb) ambaye pia ataambatana na wageni wengine mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yetu.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura ndiye mgeni rasmi Jumamosi katika Siku ya Sanaa Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
MWISHO
Tamasha hili ni la wazi yaani halina kiingilio hivyo tunawakaribisha wananchi wote wakazi wa Dar es salaam na vitongoji vyake  wafike bila kukosa kuja kuona mseto wa Sanaa na burudani na pia kuona nguvu ya Sanaa pia kutokosa pale kwenye viwanja vya kijiji cha Makumbusho tarehe 24 Septemba 2016 ,ulinzi utakuwa wa uhakika kwani tumejipanga vizuri sana na pia wapenzi wa nyama choma zitakuwapo  kwani maandalizi yake yamekamika kila kitu tulichopanga kitakuwapo bila kukosa,shughuli hii itaanza kuanzia asubuhi saa tatu hadi saa tatu usiku.

Imeandaliwa
Godfrey Mahendeka
Mkurungezi

Vigogo wa mpira wa magongo wa dunia na wa afrika watembelea ofisi za Kamati ya Olimpiki Tanzania




Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa magongo Tanzania (THA), Abraham Sykes (katikati) akimtambulisha Rais wa Shirikisho la Kimataifa la mchezo huo, Leandro Negre kwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi wakati kiongozi huyo na yule wa Afrika, Seif Ahmed walipotembelea ofisi za TOC mapema leo Alhamisi.

Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Magongo (FIH), Leandro Negre na Rais wa Afrika wa mchezo huo, Seif Ahmed leo walitembelea ofisi za Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC).

Katika ziara hiyo wawili hao waliongozana na viongozi wa mchezo huo wa kitaifa (THA), Abraham Sykes ambaye ni mwenyeki na Kaushik Doshi (Katibu Mkuu) na kufanya mazungumzo mafupi na Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akimkaribisha rais wa Chama cha Hockey cha Afrika, Seif Ahmed leo.
Ujumbe huo ukiongozwa na rais wa FIH, Leandro Negre pamoja na rais wa mchezo huo wa Afrika, Seif Ahmed wa Misri ulijadili mambo mbalimbali ya michezo na jinsi ya kuisaidia Tanzania katika mchezo huo.

Negre aliitaka TOC kuisaidia THA kupata udhamini wa mafunzo kutoka Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kupitia kitengo chake cha misaada cha Olympic Solidarity ili kupata mafunzo zaidi kwa walimu wa mchezo huo hapa nchini.
 
Mchezo wa hockey kwa mara ya kwanza ulichezwa katika Olimpiki mwaka 1908 iliyofanyika jijini London, ambapo awali ulichezwa katika viwanja vyenye majani.

Katika miaka ya 1970 walibadilisha na mchezo huo kuanza kuchezwa katika kwenye uwanja wa bandia na kuufanya kuwa wa haraka zaidi ya huko nyuma ulipokuwa ukichezwa katika viwanja vya majani.
 
Uongozi huo wa FIH juzi ulikutana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye na kuahidi kuijengea Tanzania uwanja wa kisasa wa mchezo huo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza aizawadia Sh. milioni 1 KILIMANJARO QUEENS



MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongela akiwapongeza wachezaji wa Kilimanjaro Queens walipowasili jijini Mwanza leo kabla ya kupanda ndege kwenda Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongela ameipongeza timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara, The Kilmanjaro Queens baada ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) iliyomalizika Jinja, Uganda hivi karibuni.

Timu hiyo ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kwanza ya wanawake kuandaliwa na Cecafa baada ya kuifunga timu ya soka ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Jinja, Uganda.

Katika mapokezi hayo ya timu timu hiyo mkoani hapa,Mongela alizawadia timu hiyo shilingi milioni 1 kama pongezi.

Mongela amepongeza pia Chama cha Soka cha Wanawake(Twfa) kwa juhudi zao mpaka timu hiyo imechukua ubingwa.

Mongela ameiomba timu hiyo ihakikishe inafanya juhudi kuhakikisha wanaendelea kuwa mabingwa. Mwenyekiti wa soka la wanawake nchini(TWFA) Amina Karuma ameomba makampuni yaendelee kujitokeza katika kudhamini soka la wanawake.

Karuma pia amepongeza kampuni ya Airtel na Azam kwa juhudi zao za kusaidia timu hiyo wakati ilipokuwa Uganda.

Karuma amesema ushindi huo umetokana na matunda ya michuano ya Airtel Rising Star, ambapo wameweza kupata wachezaji.

Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema michuano hiyo ilikuwa migumu sana kwa kuwa waliohofia timu za Kenya na Ethiopia kutokana zimecheza michuano ya Afcon kwa wanawake. 

"Mashindano yalikuwa magumu sana kutokana na tumefanya mazoezi ya zima moto tulijiandaa wiki moja kabla ya mashindano,kingine kilichotugharimu ni urefu wa safari kutoka Dar-es-salaam mpaka Jinja kwa bus".

Mkomwa ameomba wachezaji wawe wanaingia kambini mapema sana ili kujianda mapema katika mashindano yoyote yale.

Nahodha wa timu hiyo,Sophia Mwasikili ameiomba Serikali iwekeze zaidi katika soka la wanawake hiyo itasaidia soka la wanawake kufanya vizuri.

Mwasikili amesistiza wachezaji wawe wanajaliwa zaidi katika kupewa posho zao na mishahara kwa wakati italeta motisha kwa wao kufanya vyema.

Mfungaji kutokea timu hiyo,Mwanahamisi Omary'Gaucho' ambae amefunga magoli matatu amesema yeye aliweka malengo ni lazima ahakikishe kila mechi anafunga ili kusaidia timu yetu kufanya vyema. 

Wachezaji wa Kilimanjaro queens waliofunga magoli ni Asha Rashid magoli matatu,Donasia Donald mawili, Stumai Rajab magoli mawili.

Wachezaji walioshinda ubingwa huo ni  Fatuma Omary,Sophia Mwakisili,Anastazia Anthony,Fatuma Issa,Fadhila Hamad,Donisia Donald,Happy Hezron na Asha Rashid.

Wengine ni Wema Richard,Mwanahamisi Omari,Maimuna Hamis,Fatuma Hassan,Amina Ally,Sherida Boniface,Anna Hebron,Najat Abass na Fatuma Bashir.