Thursday, 2 April 2015

BFT yateua 17 kuunda timu ya taifa ya ndondi




Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Ndondi Tanzania (BFT) limeteua mabondia 17 watakaoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya Michezo ya Afrika na mingine ya kimataifa, imeelezwa.

Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema kuwa, mabondia hao waliteuliwa katika mashindano ya kimataifa yaliyomazika hivi karibuni kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa na kushirikisha na mabondia wa Kenya na Uganda.

Alisema kuwa mashindano hayo yaliyofanyika Uwanja wa Ndani, yalikuwa na mafanikio makubwa na yalimaliziaka Jumamosi.

Mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya tarehe 15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa.

Michezo ya Afrika itafanyika Brazzavile, Kongo kuanzia Septemba 4-19, mashindano ya ubingwa wa dunia ya Aiba Oktoba 5-18 Doha Qatar.

Mabondia waliochaguliwa kwa uzito wao ni kama ifuatavyo:-

49 kgs L/FLY
   Mohamed Mzeru JKT
   Maulid Athumani-
   Ibrahim Abdalah Magereza.

52 Kgs Fly Weight.
   Juma Ramadhani- Temeke
   Said Hofu- JKT

56 Kgs Bantam Weight
   Ahamad Furahisha- JKT
   Bon Mlingwa- JKT

60 Kgs Light weight.
   Elias Mkomwa- JKT
   Bosco Bakari- JKT
   Fabian Gaudence- NGOME

64 Kgs Light Weight

   Kassim Mbwitike- JKT

69 Kgs. Welter Weight.
   Said Gulushad JKT
   Seleman Bamtulah- JKT

75 Kgs Middle Weight.
   Ivan Mussa Kagera

81 Kgs light Heavy
   Hamidu Halfan-JKT

91 Kgs Heavy weight
   Alex Sitta- JKT
   Nuru Ibrahim- Magereza

Aidha,  BFT  inawapongeza mabondia wote kwa jitihada kubwa walizofanya na hatimae kuchaguliwa kuwa mabondia wa timu ya taifa ya ngumi 2015.

Murray, Williams wala keki kwa ushindi wa Miami Open


Keki aliyoandaliwa Serena Williams baada ya kushinda mechi ya 700.

MIAMI, Marekani
ANDY Murray atacheza na Tomas Berdych katika nusu fainali ya Miami Open baada ya kumchapa Muaustralia Dominic Thiem.

Mchezaji huyo Mscotland mwenye umri wa miaka 27 alipoteza seti ya kwanza alipokuwa akicheza na Thiem anayeshikilia nafasi ya 36 duniani, lakini alitoka nyuma na kuibuka naushindi wa 3-6 6-4 6-1.

Kwa ushindi huo sasa atakutana na mchezaji wa Jamhuri ya Czech Berdych kwa mara ya kwanza tangu aliposhinda nusu fainali ya mashindano ya Australia Open Januari.

Naye Serena Williams alipata ushindi wake wa 700 wakati akikata tiketi ya kucheza nusu fainali baada ya kumchapa Mjerumani Sabine Lisicki.

Murray anayeshikilia nafasi ya tatu kwa ubora, aliyetinga robo fainali huku akifikisha ushindi wa mechi ya 500 katika historia ya mchezo huo alipomshinda mchezaji wa Afrika Kusini Kevin Anderson,baada ya kuanza taratibu, atakutana na Thiem mwenye umri wa miaka 21.

Williams anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora duniani, alimshinda Lisicki kwa 7-6 (7-4) 1-6 6-3 na kutinga nusu fainali ya mashindano hayo.

Mmarekani huyo amekuwa mchezaji wanane kushinda mchezo wa 700 wa WTA, ingawa bado you nyuma ya Martina Navratilova mwenye mechi 1,442.

Wachezaji hao wote walikula keki kwa kushinda mechi zao, huku Murray akishindamechi ya 500 wakati mwenzake aliibuka na ushindi katika mechi ya 700.
 

Pata kwa ufupi yaliyojiri magazetini leo Aprili 02, 2015

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Mwanariadha atishiwa kifo baada ya kutoa siri za ubakaji za kocha



LONDON, England
MMOJA kati ya wanariadha mahiri katika mbio ndefu duniani na mshirika wa Mo Farah katika mazoezi amekuwa akiishi kwa wasiwasi mkubwa nchini Uganda, baada ya kutishiwa kifo kufuatia kutoa madai kuwa kocha wake alikuwa akiwanyanyasa kijinsia wanariadha wakike, wengine wenye umri wa miaka 15.

Moses Kipsiro (pichani), ambaye alifanikiwa kutetea taji lake la Jumuiya ya Madola katika mbio za mita 10,000 huko Glasgow, Scotland mwaka jana, alisema wiki hii kuwa, baadhi ya wakimbiaji wakike walikwenda kwake wakitaka msaada.

Alisema kuwa mara kwa mara amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa baada ya kuwasilisha madai hayo ya wanariadha wakike kwa Shirikisho la Riadha la Uganda na polisi.

Jumatatu Kipsiro aliwasilisha kwa polisi vitisho hivyo kupitia ujumbe mfupi wa maneno jijini Kampala, Uganda.

Mwanariadha huyo alisema kuwa anataka kuondoka Uganda yeye na mke wake na watoto watatu endapo polisi watashindwa kuchunguza madai yake. Wanatakiwa wailinde familia yangu, alisema.

Habari hiyo kwa mara ya kwanza ilipelekwa katika gazeti la Sportsmail na Pace Sports Management, ambao pia wanamuwakilisha bingwa mara mbili wa Olimpiki Farah.

Akizungumza wiki hii, mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 28 Kipsiro alisema mwaka jana alifuatwa na wanariadha watano wakike katika kambi ya mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano ya mbio za nyika za Afrika.

Kipsiro anasema kuwa walikwenda kwake kama mwanariadha mkongwe, mtu mzima na nahodha wa timu ya taifa na anayeshikilia rekodi ya taifa na alishinda medali katika kiwango cha dunia na ana medali tatu za Jumuiya ya Madola, ambapo walilalamika kuwa, kocha amekuwa akiwabaka wanariadha hao.

Moses Kipsiro amekuwa akifanya mazoezi na Mo Farah.
Kwa mujibu wa wasichana hao kocha huyo aliwaambia kuwa anataka awatie mimba na baadae kuzitoa, kwa sababu kwa kufanya hivyo kunapanua sehemu zao nyeti na kuwawezesha kukimbia kama Wakenya, aliniambia Kipsiro.

Nilikwenda katika Shirikisho la Riadha na polisi. Lakini hadi sasa hakuna chochote kilichofanyika. Mbali na kupata vitisho vya kifo, kaka yangu naye pia alitishiwa na kukamatwa.

Na hadi sasa nimetemwa katika timu ya taifa ya Uganda. Na sijakimbia katika mbio za dunia za nyika huko China wikiendi iliyopita kwa sababu yah ii tu.

Viongozi wa Shirikisho la Riadha la Uganda walipinga madai hayo lakini taarifa ya kina ilitoka katika gazeti la Uganda, ambalo lilifanya mahojiano na wanariadha watatu wakike ambao walikuwa kambi kwa miezi mitatu huko Kapchorwa Machi mwaka jana.

 Alikuja katikati ya siku na katika chumba chetu, alisema mwanariadha mmoja aliyezungumza na Daily Monitor.

Alitishia kututimua kambini endapo tungetoa siri au kumuangusha. Kambini hakukuwa na kocha mwanamke, hivyo hatukuwa na pakukimbilia…. 
Katika makala hiyo hiyo nahodha Kipsiro alikaririwa.
Nilikorofishana naye lakini matokeo yake ndio hayo, alisema. Nilichogundua kilichowahusisha wanawake ni cha kushangaza sana, kilinishtua sana,’ alisema na kuongeza:

‘Siku moja aliwakusanya wakimbiaji wa timu ya wasichana ya vijana katika maeneo ya siri na kuwaambia ili kukimbia vizuri lazima wafanye ngono au kuzaa. Nadharia yake ilikuwa hivi endapo sehemu za siri za mwanamke zitapanuka , miguu yake itakwenda haraka. Nilishtushwa kusikia upuuzi huo… 
.
`Bahati mbaya baadhi ya watu wanaamini kuwa ni kocha mzuri. Hadi sasa wanaendelea kumtetea.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha la Uganda (UAF) Beatrice Ayikoru alikaririwa katikahabari hiyo hiyo akikanusha madai hayo.

 Madai yote dhidi ya kocha ni ya uongo, alisema. Nilikutana na wanariadha huko Kampala na hakuna hata mmoja aliyezungumzia jambo hilo.

Kwa mujibu wa Pace Sports Management, ambao wana mkataba na UAF wakizungumzia suala hilo wiki hii, madai hayo yanachunguzwa na viongozi pamoja na polisi lakini bado matokeo ya uchunguzi hayajatolewa.

Wednesday, 1 April 2015

Muhammadu Buhari ampongeza Jonathani kukubali matokeo


ABUJA, Nigeria
MSHINDI wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu nchini Nigeria,  Muhammadu Buhari, amepongeza ushidi wake kama ni kura ya mabadiliko na kudhihirisha ameleta demokrasia.
Bw. Buhari pia amempongeza rais anayemaliza muda wake Goodluck Jonathan kama "mpinzani wa thamani " ambaye amekubali kushindwa katika uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi.
Jenerali Buhari alimbwaga Bw. Jonathan kwa kupata kura za ndio milioni 15 huku mpinzani wake ambaye ni rais wa sasa alipata kura milioni 12.9.
Waanfgalizi wa kimataifa kwa ujumla wamepongeza uchaguzi huo, ingawa kulikuwa na tetesi za kutokea kwa vurugu.
Bw. Buhari, wa chama cha All Progressives Congress (APC), amekuwa mgombea wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi nchini Nigeria.
Kiongozi huyo wazamani wa kijeshi katika hotuba yake leo Jumatano baada ya ushindi alielezea ushindi wake kuwa ni wa kihistoria.