Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI aliyemaliza muda wake wa Klabu ya michezo ya
Sekta ya Uchukuzi , Mohamed Ally
ameshinda kwa kishindo kwa kutetea nafasi yake katika uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika kwenye
ukumbi wa Transit wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
(JNIA-TBI) kwa kupata kura 113.
Hatahivyo, Ally pamoja na kupigiwa kura nane (8) za
hapana na sita (6) zikiharibika hakuwa na mpinzani baada ya aliyejitokeza awali Emmanuel Tumaini kujitoa dakika
chache kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mkutano wa uchaguzi.
Hassan Ahmad ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti
kwa kupata kura 71 akiwashinda Hamis Mussa (57) na Neema Makassy (8); huku
Katibu Mkuu akichaguliwa Mbura Tenga (73) aliyewashinda Katibu aliyemaliza muda
wake Alex Temba (46), Ramadhani Kalima (5) na Leonard (2).
Mrisho Harambe ameweka rekodi kwa kushinda kwa kura
124 katika nafasi ya Katibu Msaidizi ambapo zikiwa ni kura nyingi zaidi
walizopata wagombea wengine wa nafasi mbalimbali; na alimshinda Saidi Marusu
aliyepata kura nane (8).
Mweka Hazina alichaguliwa Bw. Benjamin Bikulamti (87)
aliyemshinda Wilson Magesa (42); huku wajumbe watano waliochaguliwa kutoka
katika 14 walioomba kura ni Hilda Mwakatobe (75), Kurwa Sanga (72), Burton
Willy (71), Evarist Mmanda (56) na Siraji Silimu (53).
Hatahivyo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo Mputa Maokola
amewataka viongozi wapya kudumisha ushirikiano baina yao na wachezaji, na
endapo kumetokea matatizo wahakikishe wanasuluhisha ili kuepuka vurugu.
Wasimamizi wengine kwenye uchaguzi huo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi
wa Serikali na Afya (TUGHE), Joseph Matiku kutoka Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) na Mapinduzi Ussi kutoka Mamlaka ya
Usafiri wa Anga (TCAA).
|
Akiwashukuru wapigakura kwa niaba ya viongozi wenzake, Makamu
Mwenyekiti, Ahmad amesema wanategemea mchango mkubwa wa mawazo kutoka kwa
wanamichezo hao, na kuwataka wawakosoe endapo watakuwa wanakosea.
“Kwa niaba ya wenzangu tutajituma ili kufanikisha lengo
letu la ushindi kwenye michezo mbalimbali tutakayoshiriki, lakini mtambue pia
tunategemea mchango wenu wa mawazo katika kuendeleza klabu yetu ya Uchukuzi,”
alisema Ahmad.
Mbura Tenga (mbele aliyesimama) akimwaga sera zake kwa
wapigakura wa klabu ya Uchukuzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).
|
Mbura Tenga (mbele aliyesimama) akimwaga sera zake kwa
wapigakura wa klabu ya Uchukuzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).Hata hivyo, alisema sasa watatengeneza utaratibu wa
kufanya wachezaji kukutana mara kwa mara katika michezo ya mabonanza na sio
kusubiri michezo ya Mei Mosi na Shimiwi pekee ambayo inafanyika kila mwaka mara
moja.
No comments:
Post a Comment