Na Mwandishi Wetu
MAGWIJI i wa kuonyesha
michezo kote barani Afrika – SuperSport imethibitisha rasmi kupata idhini ya
kuonEsha moja ya michuano maarufu
kabisa ya soka ulimwenguni - Kambe la
UEFA , ambapo sasa michuano hiyo itaonekana mubashara kupitia DStv na hivyo
kuwawezesha mamilioni ya watazamaji kote barani Afrika kushuhudia michezo hiyo.
Hivi karibuni, SuperSport ilishiriki katika
zabuni ya kupata idhini ya kuonyesha michuano hiyo na hatimaye kuthibitisha
kupata idhini ya kuendelea kuonyesha michuano hiyo kwa miaka mitatu ijayo
kuanzia msimu wa 2018/19.
“Hii ni siku ya Furaha na muhimu sana kwa
SuperSport na wateja wetu wote wa DStv” amesema Mtendaji Mkuu wa SuperSport
Gideon Khobane na kuongeza kuwa michuano ya UEFA ni moja ya mashindano makubwa
na yanayoshirikisha timu maarufu na wachezaji nyota wengi sana hivyo itakuwa ni
burudani ya aina yake kwa watazamaji wa DStv kote barani Afrika. Amesema kama
kawaida, kupitia DStv, watazamaji wataona michuano hiyo mubashara tena kwa
muonekano wa kiwango cha juu..
No comments:
Post a Comment