LONDON, England
NYOTA wa ndondi za uzito wa juu wa Uingereza, Anthony
Joshua anataka kujijengea umaarufu katika ndondi za kulipwa kama ule wa Roger
Federer katika mchezo wa tenisi.
Joshua hadi sasa ameshinda mapambano 20-0, yote yakiwa
kwa KO na kumpatia umaarufu mkubwa katika mchezo huo.
Bondia huyo tayari ameweka rekodi ya kuingiza watazamaji
wengi katika moja ya mapambano yake, likiwa limeingiza watazamaji 90,000 Aprili
mwaka huu alipomsimamisha Wladimir Klitschko kwenye Uwanja wa Wembley hapa.
Baadae pambano lake jingine lililofanyika mwezi uliopita,
liliingiza watazamaji 78,000, ambalo lenyewe alishinda kwa TKO dhidi ya bondia
Carlos Takam lililofanyika kwenye Uwanja wa Manispaa wa Cardiff, Wales.
Kuna wataalamu wengi wanaamini kuwa bingwa huyo wa dunia
wa WBA, IBF na IBO atakuwa mwiba mkali katika ngumi.
Federer, bingwa mara 19 wa mataji makubwa, anachukuliwa
kwa kiasi kikubwa kuwa ni mcheza tenisi mkubwa zaidi katika kipindi chote na
Joshua ana nia hiyo ya kujiweka katika nafasi hiyo.
"Sasa naelewa, natakiwa kucheza ndondi ikiwa nataka
kujijengea jina, “alisema bondia huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 28.
"Bado sijatekeleza jukumu langu. Lakini angalia
bondia kama Muhammad Ali, ambaye amekuwa alama ya mchezo wa ndondi….”
"Ikiwa unataka kuwa watu kama hawa, unatakiwa
kujibidiisha katika njia sahihi.
"Nataka kuwa kama akina [Cristiano] Ronaldos,
[Lionel] Messis, Federers anayeshindana na [Rafael] Nadal, [Andy] Murray. Hilo
nataka kulipeleka katika ngumu.”
No comments:
Post a Comment