Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imemuomba Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kuwa mgeni rasmi
katika ufungaji wa tamasha la Michezo na Utamaduni la Karatu 2017.
Tamasha hilo ambalo hushindanisha michezo mbalimbali
pamoja na ngoma za utamaduni na kwaya, litafikia kilele Desemba 23 katika
viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu.
Mratibu wa tamasha hilo, Meta Petro amesema leo kwa njia
ya simu kuwa,
Tamasha hilo ambalo huandaliwa na Filbert Bayi Foundation
(FBF) kwa kushirikiana na TOC, Chama cha Riadha Karatu na kudhaminiwa na
Olympic Solidarity,limekuwa chachu ya kuibua vipaji hasa vya riadha.
Petro anasema kuwa mbali na mbio za kilometa 10 na tano
kwa wanaume na wanawake, pia kutakuwa na mbio za kilometa 2.5 kwa watoto, mbio za
baiskeli za kilometa 60 kwa wanaume na wanawake kilometa 30, soka na mpira wa
wavu.
Anasema kuwa mchezo wa soka na wavu fainali zake
zitafanyika siku moja kabla ya kilele cha tamasha hilo, Desemba 22 na zawadi
zao zitatolewa siku inayofuata, ambapo Dk Mwakyembe ndiye atakayekabidhi zawadi
kwa washindi.
No comments:
Post a Comment