LONDON,
England
KOCHA Arsene
Wenger anasema kuwa hawezi kumuhakikishia mshambuliaji Alexis Sanchez (pichani) kubaki Arsenal
kwa muda mrefu, baada ya mshambuliaji huyo kufunga mara mbili walipocheza jana
dhidi ya Crystal Palace.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Chile anaweza kuondoka kama mchezaji huru katika kipindi
cha majira ya joto wakati mkataba wake utakapomalizika na amekuwa akihusishwa
na kutaka kuhamia kwa vinara wa Ligi Kuu ya England Manchester City, ambao
walishindwa kukamilisha usajili wa mchezaji huyo siku a mwisho ya usajili.
Alipoulizwa
kuhusu hatma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 2, kocha huyo Mfaransa
alisema: "Hakuna mtu hajuae nini kitatokea. Kwa kweli ni vigumu sana
kutabiri.
"Kwa sasa
tunaangalia mambo ya muda mfupi, hiyo ikiwa na maana mchezo ujao na wachezaji
waliojituma na ambao wako tayari kupambana. Haina uhakika utakuwe;po mahali Fulani
kwa muda gani.
"Wakati
wote wanahoji, wakati watu hawana mikataba ya muda mrefu, Njia bora ya kuonesha
jinsi watu walivyojituma ni jinsi watakavyoonesha kiwango chao uwanjani.”
Maoni yake
hayo yamekuja mwezi mmoja baada ya kuzungumza kuhusu wachezaji wote wawili, Sanchez
na kiungo Mjerumani Mesut Ozil, ambao mikataba yao ya sasa inamalizika katika
kipindi cha majira ya joto, akitaka wabaki kwenye Uwanja wa Emirates.
Jana Alhamisi,
Sanchez alifunga mara mbili katika dakika nne wakati Arsenal ikiibuka na
ushindi baada ya ndros Townsend akifuta bao la kuongoza la Shkodran Mustafi.
No comments:
Post a Comment