MADRID, Hispania
KLABU ya Real Madrid endapo itafungwa katika mchzo wao wa El
Classico dhidi ya Barcelona, basi itakuwa imetupwa nje ya mbio za kusaka
ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania ya La Liga kagika mchezo utakaofanyika wikiendi hii.
Endapo itashinda, na ikifuatiwa na ushindi mwingine kutaiwezesha timu hiyo kupunguza tofauti ya pointi
dhidi ya Barcelona
na kuwa pointi tano kabla ya mapumziko
ya kipindi cha baridi na kukipa kikosi cha Zinedine Zidane nafasi ya
kupambana.
Mpambano huo wa El
Clasico kwa timu hizo kupambana katika mpmbano wa La Liga ni wa kwanza tangu
Aprili.
Tangu walipofugwa na Real Madrid katika
mchezo wa Supercopa de Espana katika kipindi cha majira ya joto. Barca wametamba
zaidi dhidi ya wapinzani wao.
TAARIFA ZA TIMU
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez anatazamia
Gareth Bale atacheza kufuatia kufanya vvizuri katika Kombe la Klabu Duniani.
Na Cristiano Ronaldo anataka Bale kucheza
katika nafasi ya Isco kutokana na kutoelewana na Muhispania huyo wa Kimataifa.
Majeruhi Paco Alcacer hatakueemo katika
kikosi cha Barcelona licha ya kufanya kazi nzuri msimu huu katika klabu hiyo,
baada ya kufunga mabao yote katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 2-1 nyumbani
dhidi ya Sevilla.
HISTORIA YA MECHI ZAO
Mchezo huo wa Jumapili utakuwa ni wa 236 wa
kiushindani kukutana timu hizo zenye upinzani wa hali ya juu katika soka.
No comments:
Post a Comment