KLABU ya Chelsea itakuwa
na mtihani mgumu kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya baada ya
kupangwa kucheza dhidi ya Barcelona katika mchezo wa hatua ya 16 bora, wakati Tottenham itakabiliana na mabingwa wa
Italia Juventus katika mchezo mwingine wa hatua hiyo.
Vinara wa Ligi
Kuu ya England Manchester City wenyewe watakabiliana na wawakilishi wa Uswisi Basel,
Manchester United wenyewe watacheza dhidi ya timu inayoshiriki Ligi Kuu ya
Hispania, La Liga ya Sevilla na Liverpool watatoana jasho dhidi ya timu ya
Ureno ya Porto.
Mabingwa watetezi
wa Kombe la Ligi ya Mabingwa wa Afrika Real Madrid wenyewe watakabiliana na
vinara wa Ufaransa Paris St-Germain.
England imeweka
rekodi kwa kuingiza timu tano kutoka hatua ya makundi na kucheza hatua ya 16
bora msimu huu.
Celtic v Zenit,
Arsenal watacheza dhidi ya Ostersunds katika hatua ya timu 32 bora ya Ligi ya
Ulaya au Uefa ndogo kama inavyojulikana na wengi.
Chelsea ndio timu
eee ya Uingereza kufuzu hatua ya 16 bora kama mshindi wa pili swa kundi lake,
huku timu zingine nne zikiongoza katika makundi yao.
The Blues (Chelsea)
ndio inaonekana kuwa na kibarua kigumu zaidi kwa timu za Uingereza katika hatua
hiyo ya 16 bora na kuiweka katika wakati mgumu wa kuvuka hatua hiyo kutokana na
ukali pamoja na uzoefu wa Barcelona inayoongozwa na Lione Messi.
Hatua hiyo
imekuja siku chache baada ya kocha wa Chelsea Antonio Conte kusema kuwa nafasi
ya timu yake kutetea taji la Ligi Kuu imetoweka baada ya timu hiyo kupokea
kivhapo cha kutoka kwa West Ham, ambacho kimewaacha wakiwa nyuma hya Manchester
City kwa pointi 14.
Hatahivyo, Chelsea
iliifunga Barcelona katika nusu fainali kabla ya kutwaa taji la Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya mwaka 2012.
Real Madrid, ambayo
iko mbioni kutwaa taji la 13 na la tatu mfululizo, nayo imepewa timu ngumu ya
PSG, ambayo imetumia fedha kwa ajili ya usajili na imemaliza nyuma ya Tottenham katika Kundi
H.
Washindi wa
makundi watakuwa ugenini katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ya 16 bora
Februari 13 au 14 na Februari 20/21, na nyumbani katika mchezo wa marufdiano
utakaofanyika kati ya Machi 6/7 na Machi 13/14.
Fainali ya Ligi
ya Mabingwa wa Ulaya itafanyika Mei 26 Kiev,
RATIBA KAMILI YA HATUA YA 16 BORA YA LIGI
YA MABINGWA WA ULAYA:-
Juventus v
Tottenham (Februari 13 na Machi 7, 2018)
Basel v
Manchester City (Februaria 13 na Machi 7, 2018)
Porto v Liverpool
(Februari 14 na Machi 6, 2018)
Sevilla v
Manchester United (Februari 21 na Machi 13, 2018)
Real Madrid v PSG
(Februari 14 na Februaria 6, 2018)
Shakhtar Donetsk
v Roma (Februari 21 na Machi 13, 2018)
Chelsea v
Barcelona (Februari 20 na Machi 14, 2018)
Bayern Munich v
Besiktas (Februari 20 na Machi 14, 2018)
No comments:
Post a Comment