Na Mandishi Wetu,
Zanzibar
MASHINDANO ya
Kombe la Taifa ya netiboli yaliyopangwa kuanza kesho mjini Arusha, yameahirishwa
kwa sababu ya ukata, imeelezwa.
Kwa mujibu wa
Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta) Judith Ilunda, amesema leo
kwa njia ya simu kutoka jijini Dar es Salaam kuwa, mashindano hayo sasa
yatafanyika kuanzia Desemba 16 hadi 23 mjini Arusha.
Alisma awali
mashindano hayo yangeanza Desemba 10 hadi Desemba 19 na sasa baada ya
kuahirishwa yatamalizika Desemba 23 kenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Ilunda alisema
kuwa chama chake kinahitaji kiasi cha sh milioni 29 kwa ajili ya kuendeshea
mashindano hayo, ambayo hushirikisha timu za mikoa.
Alisema tayari
wamepiga hodo kwa wadau mbalimbali wakiomba wawasaidie kupatikana kwa fedha
hizo ili waweze kufanikisha mashindano hayo muhimu.
Alisema kuwa
Chaneta inakabiliwa na ukata licha ya uongozi huo mpya kukutana majukumu mengi
tangu uiongie madarakani miezi michache iliyopita mjini Dodoma.
Chaneta
ilipoingia madarakani imeendesha kwa mafanikio mashindano ya Ligi Daraja la
Kwanza yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam na
timu saba kupanda daraja.
No comments:
Post a Comment