Monday, 25 December 2017
Serikari yawakoromea Maofisa Michezo, Utamaduni
SERIKALI imesema kuwa maofisa michezo na wale wa utamaduni hawafanyi
kazi zao vizuri na ndio maana kumeshindwa kuvumbuliwa vipaji vipya na
kusababisha wachezaji wale wale kushiriki katika mashindano mara kwa mara.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza
aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifunga tamasha la 16 la Michezo na
Utamaduni la Karatu kwenye viwanja vya Mazingira Bora hapa.
Shonza alisema kuwa maofisa michezo na utamaduni wengi wao wamekuwa
wakipokea mishahara bure, kwani wameshindwa kufanya kazi zao za kusaidia kuibua
vipaji kama wanavyofanya wenzao wa Karatu kupitia tamasha hilo.
Alisema maofisa hao wanatakiwa kwenda chini hatua ya vijiji ili kuibua
vipaji na kuviendeleza tofauti na wengi wao, ambao wanapokea mishahara bure
bila ya kufanya kazi yoyote.
Aliongeza kusema kuwa ndio maana vijana wengi wamekuwa wakijihusisha na
shughuli zisizofaha kama uvutaji wa bangi, matumizi ya dawa za kulevya na wizi
kutokana na kutoshirikishwa katika michezo, hivyo aliwataka maofisa hao kufanya
kazi zao vizuri.
Pia aliwataka viongozi wa wilaya ya Karatu kuhakikisha wilayani kwao
kuna kiwanja kikubwa cha michezo ili kuwawezesha vijana kutumia kiwanja hicho
kuendeleza vipaji vyao.
Alisema ni aibu kubwa kuona wilaya ya Karatu pamoja na vipaji vya
michezo vilivypo hakuna uwanja wa maana wa michezo, hivyo aliwataka kukijenga
au kuwapokonya wale waliovamia maeneo ya wazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment