Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imevitaka
vyama au mashirikisho ya michezo kuwa na utawala bora.
Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu wa TOC,
Filbert Bayi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa kamati hiyo
uliofanyika jana katika Kituo cha Amani Welezo mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akisoma taarifa yake katika Mkutano Mkuu wa kamati hiyo leo. |
Bayi alisema kuwa ujumbe wa mwaka huu ni
Utawala Bora’ikiwa ni pamoja na uwazi ma uwajibikaji, ambapo alivitaka vyama na
mashirikisho ya michezo kuwa wa wazi katika mapato na matumizi yao.
Alisema kila mwaka wakati wa mkutano mkuu wa
TOC wamekuwa wakivitaka vyama kuwdeka wazi fedha wazipatazo pamoja na matumizi,
lakini hilo limekuwa halitekelezwi na viongozi wengi.
Mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TOC, Juliana Yassoda akifuatilia mkutano huo leo. |
Alisema wao (TOC) wamekuwa wazi kwani kila
mwaka wakati wa mkutano wao mkuu, huweka wazi kwa vyama mapato na matumizi yao
bila kificho kama ilivyoagizwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki,IOC.
Naye Rais wa TOC, Gulam Rashid alisema kuwa
TOC inapinga kabisa matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu kwani ni hatari kwa
wachezaji wetu.
Wajumbe wakifuatilia Mkutano Mkuu wa TOC leo mjini Zanzibar. |
Alisema anaipongeza Serikali kupitisha sharia
ya kupinga matumizi ya dawa hizo na kuifanya Tanzania kuwa mwanachama rasmi
katika upingaji wa matumizi ya dawa hizo.
Makamu wa Rais wa TOC, Henry Tandau akizungumza wakati wa mkutano huo. |
Rashid aliyasema hayo wakati akisoma taarifa
yake katika mkutano huo mkuu wa kawaida wa mwaka.
Aidha, alivitaka vyama kuthibitisha kushiriki
katika mikutano mikuu pamoja na ile ya Kamati ya Wachezaji (Kawata) ili kuondoa
usumbufu kwa TOC katika kupanga taratibu.
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Dk Devota Marwa akihudhuria kwa mara ya kwanza Mkutano Mkuu wa TOC tangu alipochaguliwa Septemba 30 mjini Dodoma. |
Mkutano huo pia ulijadili mambo mbalimbali
yakiwemo maandalizi ya Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kimataifa kwa
mawaka 2018 yakiwemo yale ya Jumuiya ya Madola itkayofanyika Gold Coast,
Australia.
Huo ni mkutano mkuu wa kwanza tangu kufanyika
kwa Uchaguzi Mkuu wa TOC Desemba mwaka jana mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment