Friday 1 December 2017

Allardyce asaini miezi 18 kuifundisha Everton

LONDON, England
SAM Allardyce (pichani) anasema kuwa amekubali kuwa kocha mpya wa Everton baada ya kuingia mkataba wa miezi 18 wa kuifundisha timu hiyo.

Kocha huyo alisema kuwa ni ni jambo la aina yake kuwa kocha wa timu hiyo.

Allardyce anajiunga na klabu hiyo baada ya kurejea tena England juzi, kufuatia kuwa katika mapumziko mjini Dubai, kukamilisha makunaliano na bodi ya klabu ya Everton.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 alikuwa miongoni mwa watazamaji waliofika uwanjani kushuhudia Everton ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya West Ham kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Mbali na Allardyce pamoja naye alikuwepo mmiliki Farhad Moshiri na mwenyekiti Bill Kenwright wakati timu yao ikitoa kichapo hicho kikubwa.

Sammy Lee anajiunga na klabu hiyo kama kocha msaidizi, wakati kocha wazamani wa Leicester Craig Shakespeare, ambaye alikuwa mtu wa karibu wa Allardyce wakati akiifundisha England kwa miezi minne, naye pi aataungana na benchi hilo la ufundi.

"Wakati wote nafikiri Everton ilikuwa klabu kubwa. Ni klabu kubwa kweli. Ni wazi, klabu imepitia katika hali ngumu na nina matumaini yote jayo tutaweka kando haraka na kuangali mengine.”


Mmiliki wa Everton Moshiri aliongeza: "Nimefurahi kumthibitisha Sam kuwa kocha wetu mpya. Uongozi imara utaleta ari na wachezaji wetu kufanya vizuri.”

No comments:

Post a Comment