Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
TIMU za netiboli za JKT Mbweni na Jeshi Stars zitakutana
kesho katika moja ya mechi za nusu fainali za Ligi Kuu ya Muungano kwenye
Uwanja wa Gymkhana.
Nusu fainali nyingine itawakutanisha mabingwa watetezi wa
ligi hiyo ya Muungano Uhamiaji watakaocheza dhidi ya KVZ ya Zanzibar.
JKT Mbweni imefuzu kucheza nusu fainali baada ya kuongoza
kundi lake la B na kufuatiwa na KVZ wakati Kundi A, Uhamiaji ndio wamemaliza
washindi wa kwanza wakifuatiwa na Jeshi Stars.
Katika mechi za leo Ijumaa, JKT Mbweni iliibuka na
ushindi wa mabao 41-36 dhidi ya JKT, ambapo washindi walikuwa mbele kwa 14-8,
29-18 na 34-29 katika robo ya kwanza hadi ya tatu.
Katika mchezo mwingine, Mafunzo iliibuka na ushindi wa
mabao 48-41 dhidi ya Zima Moto, huku Mafunzo wakishinda 17-7, 26-20 na 38-30
katika robo zote.
KVZ waliifunga Polisi Arusha kwa mabao 53-46, ambapo
washindi walitamba kwa 13-12, 29-21 na kufungwa 44-40 katika robo yatatu.
Katika mchezo mwingine, JKT Mbweni waliifunga Polisi
Morogoro kwa mabao 56-25 huku washindi wakishinda kwa 13-3, 28-11 na 40-19
katika robo zote tatu.
Katika mashindano hayo, Tanzania Bara imeingiza timu tatu katika nusu fainali, ambazo ni mabingwa watezi Uhamiaji, mabingwa wa Tanzania Bara JKT Mbweni na Jeshi Stars wakati zanzibar imeingiza timu moja tu ya KVZ.
No comments:
Post a Comment