Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu Tanzania Bara (VPL) mzunguko wa 12 msimu
wa 2017/2018, inaendelea leo Ijumaa baada ya kusimama kwa wiki tatu kupisha
michuano ya CECAFA Challenge Cup iliyofanyika nchini Kenya na mechi za raundi
ya pili ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).
VPL inaendelea tena leo Ijumaa usiku Desemba 29,
2017 kwa Azam FC kuikaribisha Stand United kwenye Uwanja wa Azam Complex,
Chamazi, Dar es Salaam katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa Saa 1:00 usiku.
Kesho Jumamosi Desemba 30, Lipuli na Tanzania
Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa kuanzia saa 8:00 mchana;
Mtibwa Sugar na Majimaji ya Songea zikutana katika Uwanja wa Manungu, Turiani
mkoani Morogoro wakati Ndanda itaikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda
Sijaona mjini Mtwara.
Jumapili, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara Yanga watakuwa wageni wa Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba,
Mwanza kuanzia saa 10:00 jioni huku Njombe Mji FC na Singida United
wakitangulia kwa mchezo utakaoanza 8:00 mchana Uwanja wa Saba Saba, Njombe.
VPL itakamilisha mechi za mzunguko wa 12
katika mechi zitakazopigwa mwakani, Januari mosi ambako Mbeya City wataikaribisha Kagera Sugar
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya na Mwadui wakiikaribisha Ruvu Shooting zote zikianza
kutimua vumbi kuanzia saa 10:00 jioni.
Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena
kupisha mechi za Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam
Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani, kabla
ya kuingia kwenye mzunguko wa 13 wa ligi kuanzia Januari 13 na 17, 2018.
No comments:
Post a Comment