Saturday, 2 December 2017
Uhamiaji, JKT Mbweni hapatoshi fainali netiboli Muungano
Na Cosmas Mlekani
MABINGWA watetezi wa taji la netiboli la Ligi Kuu ya Muungano, Uhamiaji
kesho itacheza na mabinga wa Tanzania Bara JKT Mbweni katika mchezo
utakaofanyika kwenye Uwanja wa Gymkhana mjini Zanzibar.
Uhamiaji walipata nafasi hiyo ya kucheza fainali baada ya kuifunga KVZ
ya Zanzibar kwa mabao 55-41 katika mchezo ulijaa msisimko kwenye uwanja huo.
Katika mchezo huo Uhamiaji ilianza vizuri badaa ya kumaliza robo ya
kwanza ikiwa mbele kwa mabao 14-7, na KVZ ikijitutumua na kulazimisha sare ya
12-12 na ile ya tatu, Uhamiaji ikarudi tena katika uongozi baada ya kumaliza
ikiwa mbele kwa 15-11.
Nayo JKT Mbweni imetinga fainali kwa mbinde baada ya kuifunga kwa tabu
Jeshi Stars pale ilipoibujka na ushindi kiduchu wa mabao 34-33 huku Jeshi Stars
wakiongoza katika robo ya kwanza kwa mabao 9-6.
Hatahivyo, JKT Mbweni walkitumia uzoefu wao na kupata ushindi wa mabao
20-15 katika robo ya pili na kushida tena katika robo ya tatu kwa mabao 27-26
kabla ya robo ya nne JKT Mbweni kushinda 34-33.
MPAMBANO WA MARUDIO
Mpambano huo wa fainali kesho utakumbusha ule wa mwezi uliopita wa Ligi
Daraja la Kwanza kwenye Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi wakati Uhamiaji
ilipotoka sare na JKT Mbweni kabla ya kufungwa na Jeshi Stars na kupoteza
ubingwa wa Bara.
Kwa hiyo katika mchezo huo wa kesho, hakuna gtimu itakayokubali kufa
kirahisi kwani kila moja itataka kudhihirisa kuwa bado wamo na haitakubali kufa
kikondoo.
Kabla ya fainali kutakuwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu wakati
KVZ itakapochuana na Jeshi Stars katika mchezo utakaofanyika kuanzia saa 8:00
Mchana.
Mashindano hayo ya Ligi ya Muungano mbali na Uhamiaji, JKT Mbweni,
Jeshi Stars na KVZ, timu zingine zilizoshiriki ni pamoja na Afya, JKU na Mundu
za Zanzibar wakati zingine ni Polisi Moro na Polisi Arusha huku Madini Arusha
ikishindwa kushiriki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment