BANGKOK, Thailand
KAWAIDA hakuna mtu ambaye hufurahia kukaa
muda mrefu katika kiwanja cha ndege, lakini imekuwa tofauti kwa familia moja ya
Wazimbabwe, ambao Kiwanja cha Ndege cha Bangkok kumekuwa nyumbani kwao kwa karibu
miezi mitatu sasa.
Kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji ya Thailand,
watoto wanne wenye umri chini ya miaka 11 na watu wazima wanne waliwasili mjini
hapa tangu Mei, lakini waligoma kurejea kwao Zimbabwe wakihofia kufunguliwa
mashtaka.
Watu hao walibainika baada ya mtu mmoja
ambaye alisema kuwa alikuwa akifanya kazi katika Kiwanja cha Ndege cha Suvarnabhumi
alipotupia picha katika mtandao wa Facebook ikimuonesha akitoa zawadi ya
Krismads kwa msichana mdogo wa kiafrika.
Kwa sasa picha bhiyo ikiwaimeondolewa, Kanaruj
Artt Pornsopit alisema familia hiyo imekuwa ikiishi kiwanjani hapo kwa karibu
miezi mitatau sasa “kwa sababu ya hali isiyo ya usalama” nchi humo.
"Natumaini wote mtarejea nyumbani kwenu
haraka iwezekanazo,”alisema.
Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Pol Col
Cherngron Rimphadee alisema familia hiyo awali iliwasili Thailand kama watalii.
Walijaribu kupanda ndege kuondoka Bangkok Oktoba kwenda jiji la Hispania la Barcelona
kupitia Kiev huko Ukraine.
Lakini walizuiwa kupanda ndege kwa sababu
hawakuwa na viza inayowaruhusu kuingia Hispania.
Hatahivyo, pia walizuiwa kuingia Thailand
baada ya awali kukaa muda zaidi kuliko viza yao ya awali ilivyokuwa ikiwaruhusu
kwa miezi mitano hivyo ilibidi kulipa faini.
Baadae familia bhiyo ilifanya utaratibu
mwingine na ndege ya Kimataifa ya Ukraine (UIA) badala yake walipitia Kiev kwenda
Dubai na baadae walipita nchi ya tatu kutaka kuingia Ulaya kama wahamiaji.
No comments:
Post a Comment