Na Mwandishi Wetu
KINYANGANYIRO cha kumsaka bingwa wa taifa wa netiboli
Tanzania kinaanza rasmi Jumapili kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini
Arusha na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Richard Kwitega ndiye anatarajia kuwa geni rasmi katika ufunguzi huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta),
Judith Ilunda amesema kuwa, ufunguzi rasmi utafanyika Jumapili na timu za mikoa
ya Morogoro na wenyeji Arusha ndio itafungua mashindano hayo.
Ilunda amesema kuwa mechi ya pili Jumapili ni ile
itakayozikutanisha timu za mikoa ya Dodoma na Kilimanjaro, ambay ndio
italayofunda dimba siku hiyo.
Amesema kuwa mechi za mashindano hayo zinatazamiwa
kuanza Jumamosi kabla ya ufungizi rasmi Jumapili, ambapo kutakuwa ne mpambano
kati ya Kigoma watakaocheza dhidi ya Arusha kuanzia saa 8:00 mchana, huku mkoa
wa Songwe ukitoana jasho na Kigamboni kabla ya Morogoro haijapepetana na
Kagera.
Ilunda anasema kuwa hadi sasa jumla ya mikoa 12
ilikuwa imethibiisha kushiriki mashindano hayo yanayotarajia kumalizika Desemba
23 mwaka huu, ambapo washindi watakabidhiwa zawadi zao vikiwemo vikombe na
vyeti vya ushiriki.
Anasema kuwa uongozi wake ambao uliingia madarakani
Septemba 30 mjini Dodoma, unaendesha mashindano kwa shinda kutokana na ukosefu
wa fedha nan i matumaini yao kuwa wadau wa netiboli ikiwemo Serikali
itawasaidia kufanikisha majukumu yao.
Awali, mashindano hayo yalipangwa kuanza Desemba 10,
lakini yaliahirishwa kutokana na Chaneta kushindwa kupata zaidi y ash milioni
20 kwa ajili ya kuendeshea mashindano hayo ya Taifa Cup.
Hivi karibui Chaneta iliendesha kwa mafanikio makubwa
mashindano ya Ligi Daraja la Pili Taifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya
Kikwete Jijini Dar es Salaam, ambapo timu saba zilipanda daraja.
No comments:
Post a Comment