Friday, 1 December 2017

Wenger ahofia Mourinho kupaki basi kesho

LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger hatarajii kabisa Jose Mourinho wa Manchester United kuegesha basi wakati watakapocheza na Arsenal leo kwenye Uwanja wa Emirates.

Timu hizo mbili zinakutana katika mchezo huo kila moja ikiwa imeshinda mechi tatu mfululizo za Lig Kuu, huku Man United ikiwa na pointi nne zaidi juu ya Arsenal klatika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.

United inaangalia kushinda ushindi wake wa kwanza katika majaribio nane dhidi ya wapinzani wake waliokatika bafasi sita za juu chini ya Mourinho,wakitoka sare mara tatu na kupoteza mara nne katika mechi saba zilizopita huku wakifunga mara moja tu.

Alipoulizwa kama anatarajia Mourinho atapaki basi, Wenger alijibu: "Hapana, Sitarajii kitu chochote maalum. Natarajia sisi kupambana na hali yoyote.

"Man Utd ni timu ngumu na ninatarajia sisi kuenda sambamba na matatizo yatakayotokea dhidi yetu. Watashambulia vizuri. Na sio kama watajilinda tu.

"Ni mchezo kati ya Arsenal na Man United nyumbani [the Emirates]. Ninachotaka ni kuelekeza nguvu katika mchezo huo na kuiandaa timu yangu vizuri, na kuipa timu yangu nafasi nzuri ya kushinda.

"Kwa sasa Man Utd inakwenda vizuri, na sisi tunafanya vizuri kwa sasa, hivyo utakuwa mchezo wenye ushindani wa hali ya juu.”

Mchezo huo umekuja katika kipindi kizuri katika msimu kwa Arsenal, kufuatia ushindi wa London derby dhidi ya Tottenham,na baadae dhidi ya Burnley na ule wa 5-0 Jumatano dhidi ya Huddersfield.

Hatahivyo, Wenger ana majeruhi kibao katika kikosi chake, pamoja na mshambuliaji Alexandre Lacazette aliyebadilishwa wakati wa mapumziko walipochea dhidi ya Huddersfield kutokana na maumivu ya nyomga.

Majeruhi mwingine ni Alexis Sanchez ambaye pia ilibidi kubadilisha baadae kutokana na kuhisi maumivu ya nyama za paja.


Wenger anatarajia Sanchez kuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo lakini tayari amekata tamaa na Lacazette, ikiwa na maana kuwa Olivier Giroud ataanza mchezo wa kwanza wa ligi kufuatia  ushindi wa mabao mawili dhidi ya Huddersfield.

No comments:

Post a Comment