KAMPALA, Uganda
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda Emmanuel Okwi
aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Ligi Kuu ya Denamark ya SønderjyskE, amejiunga
na klabu ya Sports Club Villa ya nchini kwao Uganda.
Mshambuliaji huyo aliyeanza maisha yake ya soka
kwenye klabu ya Sports Club Villa anarejea kwenye klabu hiyo kwa mkataba wa
muda mfupi ambao utamfanya achezee klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Okwi aliondoka
SC Villa na kujiunga na Simba mwaka 2010
baada ya kuisaidia timu hiyo ya Uganda kushinda taji la nchi hiyo mwaka 2009.
“Usajili wake
umekamilika,” alithibitisha Mkurugenzi Mtendaji wa klabu hiyo, Ivan Kakembo .
Usajili wa mshambuliaji huyo kunaweza kuwa pigo kwa
klabu ya Simba ambapo iliriafiwa kuwa na mpango wa kumrejesha kuimarisha safu
ya ushambuliaji ya timu hiyo kwa msimu ujao.
Hata hivyo Simba bado inaweza kumpata mshambulaji
huyo mwishoni mwa msimu huu kama hataamua kusaini kusaini mkataba mpya na klabu
hiyo pindi mkataba wake wa sasa utakapomalizika na Simba kama bado itaendelea
kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo.
Wakati Okwi akirejea kwenye klabu yake ya zamani ya
Sports Club Villa, swahiba wake mkubwa Hamisi Kiiza’Diego’ aliyewahi kutamba na
mabingwa wa soka wa Tanzania Bara Yanga kabla ya kutimkia Simba nae amerejea
kwenye klabu yake ya URA huko huko Uganda.
Kiiza amejiunga na URA akitokea klabu ya Free State
ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo Agosti mwaka jana baada ya kumaliza mkataba
wake na klabu ya Simba, pia amesaini mkataba wa muda mfupi utakaomuweka kwenye
klabu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu.
“Najisikia
vizuri kurudi nyumbani,” alisema Kiiza. “Nina kumbukumbu nyingi nzuri kwenye
klabu hii na niko hapa kulipa shukrani kwa imani yao kwanguI,”aliongeza.
Kiiza alisema kuwa alikuwa na ofa nyingi kutoka ndani
na nje ya Uganda lakini aliamua kurejea kwenye klabu aliyodai iko ndani ya moyo
wake.
.
No comments:
Post a Comment