Monday 6 February 2017

maguvu ya cameroon yawapa ubingwa afcon 2017 baada ya kuwakandamiza mabingwa mara saba Misri 2-1



BRAZAVILLE, Gabon
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Cameroon, Hugo Broos ameufananisha ushindi wa timu yake kuwa ni dhidi ya timu yenye mbinu nyingi ya Misri na hatimaye kutwaa taji la Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Cameroon ilitwaa ubingwa huo dhidi ya washindi mara saba wa taji hilo katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade de l’Amitie mjini hapa juzi.
Kocha huyo Mbeligiji alikiri kuwa Simba hao wasiofungika katika dakika 45 za mwanzo ilipambana katika kiungo lakini baada ya majadiliano ya kiufundi wakati wa mapumziko walitatua matatizo yote ya awali.

“Kiukweli hatukuwa vizuri kifundi katika kipindi cha kwanza kwa sababu Misri walitawala katika kiungo.
Nilijaribu kuwaambia wachezaji lakini hawakuelewa hivyo nilisubiri hadi kipindi cha mapumziko kuwaelezea, “alisema Broos.
 
Mchezaji anayeichezea Arsenal, Mohamed Elneny ndiye aliyeipatia Misri bao la kuongozakatika dakika ya 21 baada yakufunga bao safi dhidi ya kipa wa Cameroon Fabrice Ondoa na kuwafanya Misri kwenda mapumziko wakiwa mbele.

Hatahivyo, ari alirejea katika timu ya Cameroon katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili na kujenga msingi imara wa mashambulizi wakati wakifikiria kusawazisha.
“Wakati wa mapumziko, niliwaonesha wachezaji nini chakufanya na kwa kweli walifanya kile nilichowaelekeza. Kinguvu tulikuwa bora zaidi ya Misri na hiyo ndio sababu tulishinda mchezo ule.”

Cameroon sasa imeshinda taji hilo mara tano ikiwemo lile la miaka 1984, 988, 2000, 2002 pamoja na mwaka huu kabla ya fainali za Afcon 2019 kufanyika mwakani nchini mwao.

No comments:

Post a Comment