Thursday, 9 February 2017

Kocha Wenger bado auota ubingwa ligi kuu england



LONDON, England
ARSENAL inatakiwa kuamini kuwa bado inaweza kushinda taji la Ligi Kuu ya England msimu huu licha ya kuwa nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi 12, anasema Arsene Wenger.

The Gunners, ambao kwa mara ya mwisho walitwaa taji hilo la ligi mwaka 2004, iliteleza hadi katika nafasi ya nne baada ya Jumamosi iliyopita kupokea kichapo chamabao 3-1 kutoka kwa Chelsea.

Kikosi cha kocha Wenger Jumamosi kitaikaribisha Hull City ambao wamepoteza mechi zao tisa za zilizopita za ligi.

"Bado mbio hazijamalizika, “alisema kocha huyo Mfaransa. "Hata kama nyinyi [waandishi] mnafikiri mbio za ubingwa zimeshamalizika, Sifikiri hivyo, kamwe hatuwezi kufikiria hivyo.”

Ni pointi tano tu zinatutofautisha na Tottenham iliyopo katika nafasi ya pili kutoka kwa Manchester United iliyopo katika nafasi ya sita.

Wenger aliongeza: "Tuko katika mbanano na mpambano wa kila nafasi ni mgumu sana, labda huenda ukawa zaidi kuliko huko nyuma.
"Endapo ukiwa umemalizika kwetu, bsi utakuwa umemalizika kwa kila mmoja wakati wote tukiwa katika kundi moja.

"Chelsea wana faida zaidi, wenyewe hawachezi katika mashindano ya Ulaya, hawachezi mechi za katikati ya wiki na wako katika nafasi nzuri.”

'Tunatakiwa kuungana au la sivyo hatutakuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa'
Kipigo cha Arsenal kutoka kwa Chelsea kilikuja siku nne baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 2-1 nyumbani kutoka kwa Watford.
 
Tayari baadhi ya mashabiki wanataka Wenger kuondoka, ambapo mmoja katika Uwanja wa Stamford Bridge alibeba bango likimwambia Mfaransa huyo: "Inatosha. Ni muda wa kuondoka.”

No comments:

Post a Comment