JOHANNESBURG, Afrika Kusini
BARAZA la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika (Cosafa) limesema litamuunga
mkono Ahmad Ahmad (pichani) katika uchaguzi ujao wa kiti cha urais katika Shirikisho la
Soka la Afrika (Caf).
Ahmad, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa Chama cha Soka cha Madagascar, tayari
alishatangaza nia yake ya kumpinga kiongozi wa muda mrefu wa Caf Issa Hayatou katika
uchaguzi utakaofanyika Machi nchini Ethiopia.
Cosafa ilitangaza msimamo wake huo wa kumuunga mkono Ahmad kufuatia
mkutano wa marais wa vyama vya soka vya nchi za kusini mwa Afrika uliomalizika
jijini hapa Jumamosi.
Katika taarifa yake, Cosafa ilitangaza kuwa watamuunga mkono kwa asilimia
100 mjumbe wao huyo katika uchaguzi wa Caf na Fifa, Shirikisho la Kimataifa la
Soka.
"Huu ni mkutano wetu wa kwanza tangu kamati mpya ya utendaji
ilipochaguliwa na tunafurahi na maamuzi yaliyochukuliwa na Barazala ambao
utabadili sura ya soka katika ukanda wetu, “alisema Rais wa Cosafa Phillip
Chiyangwa.
Issa Hayatou, ambaye amekuwa rais wa soka la kiafrika tangu mwaka 1988, anasaka
kuongoza kipindi cha nane Caf.
Mcameroon huyo alichaguliwa tena bila kupigwa wakati wa uchaguzi wa
mwisho uliofanyika mwaka 2013.
Awali alitangaza kuwa kipindi hiki kitakuwa cha mwisho kwake hadi pale
walipobadilisha taratibu.
Mwaka 2015, Caf ilipiga kura kubadili utaratibu, ambapo viongozi
hawaruhusiwi kugombea endapo watakuwa na zaidi ya umri wa miaka 70.
No comments:
Post a Comment